Vitambulisho vya wajasiriamali sasa kutumika kukopa benki

0

Rais Dk. John Magufuli amesema miaka mitano ijayo vitambulisho vya wajasiriamali vitaboreshwa na kuwekwa picha zao na wataweza kuvitumia kupata mikopo Benki.

Magufuli ametasema hayo leo Ijumaa Novemba 13, 2020 wakati akizindua Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma.

“Katika miaka mitano ijayo tunakusudia kuviboresha vitambulisho vya Wajasiriamali kwa kuviongezea picha ili Wafanyabiashara wadogo watambulike na kuwawezesha kupata mikopo benki, lengo ni kufanya wakue kibiashara,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here