Viongozi wa Ulaya, Uingereza kuendeleza majadiliano ya Brexit

0

LONDON, UINGEREZA

VIONGOZI wa kamisheni ya Umoja wa Ulaya na Uingereza watajaribu kutupa kete ya mwisho ya makubaliano ya kibiashara ya baada ya Brexit, huku pande zote zikionya kwamba uwezekano wa kufikia makubaliano mwishoni mwa mwaka unafifia.

Ofisi ya waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson imethibitisha kwamba waziri mkuu huyo na rais wa kamisheni ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen wataendelea na majadiliano kuhusu mustakabali wa kimahusiano kati ya Uingereza na umoja huo, katika chakula cha jioni mjini Brussels.

Mkutano huo unafanyika siku moja kabla ya mkutano wa kilele wa siku mbili utakaofanyika mjini humo kuanzia kesho Alhamisi, ambao Umoja huo unaamini kwamba hautagubikwa na kiwingu cha Brexit.

Zikiwa zimesalia takriban wiki tatu za kufikia ukomo wa muda uliowekwa kwa Uingereza kujitoa rasmi kwenye Umoja wa Ulaya, bado kuna masuala tete matatu yanayokwamisha kufikiwa kwa makubaliano.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here