Home Uncategorized Vigogo wawili wa Takukuru Tanga wasimamishwa kazi

Vigogo wawili wa Takukuru Tanga wasimamishwa kazi

Kaimu Mkurugenzi wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Mbungo

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) nchini Tanzania imewasimamisha kazi watumishi wawili wa taasisi hiyo kupisha uchunguzi dhidi yao.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Ijumaa Machi 20, 2020 na Kaimu Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Brigedia Jenerali John Mbungo imewataja watumishi waliosimamishwa ni mkuu wa Takukuru mkoa wa Tanga, Christopher Mariba na ofisa uchunguzi mkuu wa Takukuru mkoa wa Tanaga, Hilton Njau.

Taarifa hiyo imesema watumishi hao wamesimamishwa kutokana na kuhusishwa na tuhuma za kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa mmoja wa watuhumiwa waliokuwa wakichunguzwa.

“Ili kuhakikisha chombo hiki hakichafuliwi, ipo sera ndani ya chombo hiki ya kutomvumilia mtumishi yoyote anayetuhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa, hivyo basi kwa msingi huo, watumishi wamesimamishwa kazi kuanzia leo Machi 20, 2020 kupisha uchunguzi dhidi yao na uchunguzi huo utakapokamilika hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Kutokana na kusimamishwa kazi kwa Mariba, Dk Sharifa Bungala ameteuliwa kukaimu nafasi hiyo “wakati uchunguzi huu ukiendelea,  nimemteua  Dk  Sharifa  Bungala kukaimu nafasi ya Mkuu wa Takukuru mkoa wa Tanga kuanzia leo Machi 20,2020,” imesema taarifa hiyo. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -

Most Popular

Yanga yampatia Tshishimbi mkataba mpya

NA MWANDISHI WETU Klabu ya Yanga SC, imesema kuwa tayari imemaliza kazi yake ya kuhakikisha inambakiza kiungo tegemeo wa...

Tetesi za soka barani Ulaya

SANCHO AITIKISA UNITED Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Timu ya Taifa ya Uingereza, Jadon Sancho (20), amesema hatakuwa tayari...

Makonda: Wazururaji hawatakwenda mahabusu watazibua mitaro ya maji machafu

NA MWANDISHI WETU Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema kuwa watu watakaokamatwa kwenye mkoa huo kutokana...

Chui katika hifadhi ya wanyama ya Bronx akutwa na Virusi vya Corona

NEW YORK, MAREKANI Chui wa kike wa Malaysia aliyefahamika kwa jina la Nadia mwenye umri wa miaka minne katika hifadhi...

Recent Comments