Vifo vya ajali za ndege vimeongezeka licha ya kupungua kwa safari za anga

0

BERLIN,UJERUMANI

Taasisi yenye kufanya tathmini za ajali za ndege ya JACDEC, yenye makao makuu yake mjini Hamburg Ujerumani imesema idadi ya watu waliokufa kutokana na ajali za ndege imeongezeka kwa mwaka 2020, pamoja na kupungua kwa kiwango kikubwa kwa idadi ya wanaosafiri kwa njia hiyo kutokana na janga la virusi vya corona.

 JACDEC imesema kwa mwaka 2020 jumla ya watu 318 wamekufa, ikiwa ni ongezeko la watu 25 ikilinganishwa na mwaka 2019.

Matokeo yanaonesha hivyo ingawa matukio ya ajali za ndege pia yamepungua kwa mwaka huu, kwa kutokea mikasa tisa tu, na 2019 yalikuwa 27.

 Ripoti hiyo pia imeongeza kusema idadi kubwa ya vifo ilichangiwa na matukio mawili makubwa ya ajali, likiwemo lile la kuangushwa kwa ndege ya abiria ya Ukraine, lililotokea Januari nchini Iran na ajali ya ndege nyingine ya kibishara, Mei iliyokea Karachi, Pakistan.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here