Vanessa Mdee karibuni kuitwa mama

0

Na Mwandishi Wetu

PAMOJA na mwanadada Vanessa Mdee kukanusha taarifa za kuwa mjamzito kwa sasa lakini ameweka wazi kwa mashabiki zake kuwa moja ya mipango yake na mpenzi wake Rotimi ni kupata mtoto hivi karibuni.

Vanessa ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani huku kukiwa na sintofahamu ya kuendeelea na muziki wake alizungumza Live kupitia Youtube Chanel yake na kusema si kweli kuwa yeye ni mjamzito kwa sasa.

“Kumekua na habari nyingi kuhusu mimi, zinazohusu kuacha muziki na hata kuwa mjamzito, labda hili la kupata mtoto niweke wazi kuwa sina ujazito lakini mipango yetu ya sasa ni mimi na mpenzi wangu kuwa kwenye mipango hiyo”alisema Vanessa.

Aidha Vanessa alikiri kuwa ni kweli amekua kimya katika sekta nzima ya muziki lakini mashabiki zake wanapaswa kufahamu kwa sasa amekua na mambo mengo ikiwemo suala zima la kuingia mikataba na makampuni tofauti nchini Marekani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here