Vanessa Mdee avishwa pete ya uchumba

0
Penzi la mwanamuziki Vanessa Mdee na muigizaji wa Marekani mwenye asili ya Nigeria limezidi kunoga baada ya Rotimi kumvisha pete ya uchumba dada yetu usiku wa kuamkia leo Desemba 31.Kupitia video iliyopostiwa kwenye ukurasa wa Instagram wa The Shade Room, anaonekana Rotimi akiwa amepiga goti, huku akimuomba Vanessa akubali kuvishwa pete hiyo, ambapo Vanessa alikubali huku akilia kwa furaha.

Baada ya video hiyo, pia ilichapishwa video nyingine ikiwaonyesha wawili hao na watu wao wa karibu wakipata chakula cha jioni kisha Vanessa alionyeshea pete vizuri zaidi kwa kuisogeza karibu na kamera.

Vanessa amethibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameweka video mbili moja ikionesha pete aliyovishwa huku nyingine ikiwa ni kipande cha video ya mahojiano aliyowahi kufanya na moja ya vyombo vya habari na kusema ilimgharimu siku mbili tu kujua kwamba Rotimi ndiye atakayekuja kuwa mume wake.

“Mwaka mmoja na nusu uliopita dunia ilicheka niliposema kuwa nilijua kuwa wewe utakuja kuwa mume wangu muda mfupi baada ya kukufahamu, sikuwalaumu kwani hisia unayoipata pale unapokutana na mpenzi wa maisha yako si ya kawaida na haiwezi kuelezeka lakini pia wao walikuwa wakimfahamu Vanessa ambaye hakuwa na mpango wa kuolewa kwa wakati huo,” ameandika Vanessa.

Rotimi naye kupitia ukurasa wake wa Instagrama ameweka video fupi ya pete aliyomvalisha Vanessa akiambatanisha na ujumbe unaoelezea namna anavyompenda mrembo huyo.

“Unanifanya niwe mwanaume bora. Nina deni kwa Mungu kwa kunipa wewe na nitamlipa kwa kukupenda na kukupa kila kitu unachostahili, nakupenda,” ameandika Rotimi.

Uhusiano wa wawili hao ulianza mwaka 2019 baada ya Vanessa kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, mwanamuziki wa Tanzania, Jux.

Kwa sasa Vanessa ambaye mwezi Juni alitangaza kuachana na shughuli za muziki anaishi Marekani pamoja na mwanume huyo na mara kadhaa amekaririwa akimsifia kuwa ni mwanaume aliyefanya aitambue thamani ya maisha yake.

Kwenye moja ya ‘podcast’ zake za Deep Dive with Vanessa, Vee Money alifunguka; “Rotimi amenifanya nijue thamani yangu. Kabla ya kukutana tulikuwa na maisha huko nyuma, lakini ni kama hayahesabiki tangu tumeanza haya maisha yetu mapya, hususan vitu hasi.”

Rotimi ambaye jina lake kamili ni Olurotimi Akinosho, ni mwanamuziki na muigizaji. Anamiliki ngoma kali kama vile Meeting In My Bed na Love Somebody. Pia amecheza kwenye tamthilia maarufu ya Power na filamu ya Divergen

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here