UVCCM PUGU STATION WATOA VYETI VYA SHUKRANI KWA MAKUNDI MBALI MBALI YA VIJANA

0

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Pugu Station Chini ya Mwenyekiti wake Ndugu Juma Mizungu umetoa vyeti vya shukrani kwa vijana wa Hamasa pamoja na makundi mbalimbali ya vijana walio shiriki shughuli ya kampeni za mwaka 2020.

Makundi hayo ni kama ifuatavyo;
1. Bodaboda
2.Camp za Vijana
3. Vijana wa Hamasa
4. Wasanii
5. Chipukizi

Sambamba na hilo Umoja wa Vijana Kata ya Pugu Station uliweza kuwatunuku Vyeti vya pongezi Wenyeviti wa Serikali ya Mtaa wawili pamoja na Diwani wa Kata hiyo kwa kugombea nafasi za Serikali na kushika dola kwani Viongozi hao ni zao la Umoja wa Vijana Kata ya Pugu Station.

Katika hafla hiyo ya kukabidhi vyeti vya shukrani Mgani Rasmi alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Wilaya ya Ilala Komredi Hamad Pazi

Mwenyekiti wa Vijana Wilaya ya Ilala Komredi Hamad Pazi aliwapongeza Viongozi wa Kata ya Pugu Station kwa kutoa vyeti vya Shukrani kwa makundi ya vijana walio shirikiana nao katika Kampeni za Mwaka 2020.

Komredi Hamad Pazi alimalizia kwa kutoa Darasa la Itikadi kwa Vijana wote walio fika katika hafla hiyo huku akiwataka kuendelea kukipenda Chama Cha Mapinduzi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here