Mahakama Kuu ya Marekani imekataa jaribio la kutotambua matokeo ya Uchaguzi Mkuu katika Majimbo manne, licha ya Rais Donald Trump kushinikiza suala hilo
Kesi hiyo iliyowasilishwa wiki hii ilitaka kubatilisha matokeo ya Georgia, Michigan, Pennsylvania na Wisconsin ambapo Rais Mteule, Joe Biden alitangazwa mshindi
Madai hayo yaliungwa mkono na Wanasheria Wakuu 18 pamoja na Wanachama wa Republican 106 kutoka Congress
Kamati ya Uchaguzi inatarajiwa kulutana Jumatatu na kumchagua rasmi Biden kuwa Rais wa 46 wa Marekani