Urusi yapeleka askari 300 Afrika ya Kati

0

MOSCOW, URUSI

URUSI imetuma askari wa ziada 300 wa mafunzo katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati (CAR) kukabiliana na kile Wizara ya mashauri ya kigeni ya nchi hiyo imesema “kushuka kwa kiwango cha usalama kwa hali ya juu “.

Inasema serikali ya CAR , ambayo inatishiwa na makundi ya waasi kabla ya uchaguzi wa Jumapili wa urais, ilikuwa imeomba usaidizi.

Rais wa zamani wa nchi hiyo François Bozizé alikausha kufanya njama za mapinduzi.

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa walisema mashambulio ya waasi yamezimwa.

Naibu waziri wa mambo ya nje wa Urusi Mikhail Bogdanov alisema kuwa wanajeshi wa Urusi hawahusiki katika mapigano katika CAR na kwamba watoa wakufunzi wa kijeshi “sio wanajeshi wala kikosi maalumu”.

Lakini msemaji wa serikali alinukuliwa na shirika la habari la AFP akisema Urusi imetuma “mamia kadhaa ya wanajeshi na silaha nzito ” nchini humo kuunga mkono serikali.

Msemaji huyo , Ange Maxime Kazagui, alisema kuwa Urusi ilialikwa kama sehemu ya makubaliano ya ushirikiana, limeripoti shirika la habari la AFP.

Walinzi binafsi wa Urusi walikuwa wakifanya kazi katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati kutoa ulinzi kwa serikali na kusaidia kulinda mali muhimu za kiuchumi.

Takriban wanajeshi 750 wa Rwanda na maafisa wa polisi wamekuwa wakifanyia kazi nchini humo chini ya kikosi cha walinda amani cha Umoja wa Mataifa kinachojulikana kama Minusco.

Rwanda imepeleka kile inachokiita “kikosi cha ulinzi ” katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati baada ya walinzi wake wa amani kushambuliwa na waasi katika mji mkuu, Bangui.

Rais wa Rwanda Paul Kagame alisema kwamba nchi yake iliamua kutuma askari katika Jamuhuri ya Afrika ya kati ili kulinda askari wa nchi hiyo waliomo katika kikosi cha umoja wa mataifa ambao wamekuwa wakilengwa na wanamgambo wenye silaha.

Rais Faustin Archange Touadéra alisisitiza kuwa uchaguzi wa Jumapili utaendelea kama ulivyopangwa, akisema kuwa uwepo wa walinda amani wa Umoja wa Mataifa unamaanisha kuwa watu hawana la kuogopa.

Lakini vyama vya kisiasa vya upinzani, kikiwemo cha Bozizé, vimetoa wito wa kuahirishwa kwa uchaguzi “hadi amani na usalama vitakapopatikana “.

Makundi ya waasi yamechukua udhibiti wa miji kadhaa iliyopo karibu na mji mkuu Bangui , huku wakikabiliana na vikosi vya usalama na kupora mali, na Umoja wa Mataifa ulisema kuwa wanajeshi wake wanafanya hima kuleta amani Bangui.

Msemaji wa Bozizé Christian Guenebem alisema : “Tunakanusha kabisa kwamba Bozizé ni chanzo cha kila kitu

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here