Urusi yafungua uchunguzi mpya dhidi Navalny

0

MOSCOW, URUSI

Wachunguzi wa umma nchini Urusi wamesema wamefungua mashtaka mapya ya jinai dhidi ya Alexei Navalny ambaye ni mkosoaji mkubwa wa serikali nchini humo. Navalny ameilezea hatua hiyo kuwa ni kichekesho.

Wapelelezi hao wanamtuhumu Navalny na washirika wake ambao hawakutajwa, kwa kutumia takriban dola milioni 5 kwa mahitaji binafsi ilhali ni misaada ya umma kwa mashirika anayosimamia.

Kamati ya uchunguzi imeeleza kwamba Navalny alizitumia fedha hizo kwa kununua vifaa vyake binafsi na kuhudumia likizo zake binafsi nje ya Urusi. Akikutwa na hatia, Navalny huenda akahukumiwa hadi kifungo cha miaka kumi jela kulingana na sheria ya Urusi.

”Navanly anaweza kurejea nyumbani”

Wakili wa Navalny amesema kuwa viongozi wa Urusi walimtaka Navanly kurejea nchini kabla ya Jumanne ya Desemba 29. Mamlaka ya Magereza imemshutumu Navalny kwa kukiuka masharti ya hukumu ya kifungo ambacho bado anatumikia tangu mwaka 2014. Urusi ilidai kwamba Navalny anaweza kurejea nyumbani kama raia wengine.

”Kila raia wa Urusi yuko huru kurejea nchini. Na hakuna vizuizi kwa yeyote yule. Kuhusiana na hali ilivyo nadhani ni bora kwa mamlaka ya magereza ambayo ilitoa ilani hiyo kutoa taarifa.”

Hatua hiyo huenda ikatizamwa kama ishara ya hivi karibuni ya Urusi kumkamata Navalny ambaye anaendelea kupona nchini Ujerumani baada ya jaribio la kuuawa kwa kuwekewa sumu mwezi Agosti.

Kwenye mtandao wake wa Twitter, Navalny aliandika kwamba hatua hiyo inaonesha kwamba Rais Vladmir Putin anakumbwa na jazba dhidi yake. Huku akiwatolea mwito wafuasi wake kupuuza uchunguzi huo ambao aliuita kuwa hatua ya kichekesho na kuwaomba waendelee kuchangia misaada kwa ajili ya mashirika yake.

Mpinzani huyo wa Rais Putin amesema uchunguzi dhidi yake, unatokana na kashfa ya sumu aliopewa mwezi Agosti. Navalny ni miongoni mwa wakosoaji wakubwa wa Rais Putin. Hata hivyo Urusi ambayo imepinga madai ya kumtilia Navalny sumu, imesema yuko huru kurejea nyumbani.

Navalny alisema wanataka kumtupa jela kwa sababu walishindwa kumuuwa na kwa sababu amekuwa akichunguza kuhusu watu waliopanga njama ya kumuuwa.

Hii leo, Urusi imetangaza kuwawekea vikwazo baadhi ya viongozi wa Uingereza, kuhusiana na tuhuma za kupewa sumu Navalny. Uingereza, Marekani na Umoja wa Ulaya iliishutumu Urusu kuumpa sumu mpinzani huyo wa Putin.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here