Ulimwengu ang’aa TP Mazembe

0

KINSHASA, DR CONGO

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars na Klub ya TP Mazembe ‘Kunguru wa Katanga’ ya Congo, Thomas Ulimwengu amezidi kung’aa katika Ligi Kuu ya Congo baada ya kuipatia ushindi timu yake ya TP Mazembe wa goli 1-0 dhidi ya Dauphin Noir.

Goli hilo la Ulimwengu linamfanya afikishe jumla ya magoli manne katika Ligi Kuu ya Congo msimu wa 2020/21 akiwa nafasi ya pili kwa vinara wa magoli wa kwanza akiongoza kwa kuwa na magoli 5 katika Ligi Kuu Congo (Ligue 1).

Ulimwengu sasa toka arejee TP Mazembe baada ya kuwa na kiwango cha kupanda na kushuka sababu ya jeraha la goti, sasa amerejea katika uwezo wake na kuwa tumaini kwa TP Mazembe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here