Ujerumani kuweka masharti mapya kukabiliana na corona

0

BERLIN,UJERUMANI

NCHINI Ujerumani mabaa na maeneo mengine ya kuuza vileo yatafungwa. Mikusanyiko ya kijamii pia itapunguzwa kwa kiasi kikubwa.

Hatua hizo ni kati ya msururu wa masharti mapya kwa ajili ya kupambana na virusi vya corona. Serikali inajaribu kusitisha viwango vya maambukizi vinavyoongozeka.

Mipango hiyo itawasilishwa leo wakati Kansela Angela Merkel atakapofanya mkutano wa video na mawaziri wakuu wa majimbo 16 ya nchi.


Chini ya kanuni hizo mpya, ambazo huenda zikaanza kutekelezwa Novemba 4 hadi mwisho wa mwezi huo, watu wataruhusiwa tu kukutana katika maeneo ya umma na jamaa zao wanaoishi katika nyumba moja na kaya nyingine moja.

Mabaa, vilabu na maeneo ya aina hiyo yatafunguliwa tu kwa ajili ya huduma za kununua bidhaa za kufungiwa.

Shule  na vituo vya malezi ya watoto vitaendelea kutoa huduma lakini chini ya kanuni mpya za usafi. Tangu kuanza kwa janga la corona, watu wapatao 450,000 wameambukizwa nchini Ujerumani na zaidi ya watu 10,000 wamefariki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here