NA MWANDISHI WETU
HATIMAYE ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na Watanzania imefika. Jumatano ambayo inahitimisha safari ya miezi miwili ya wagombea Urais, Ubunge na Udiwani kujinadi na kuitangaza ilani ya vyama vyao. Katika wagombea wote, Rais John Magufuli ndiye mgombea pekee aliyeeleza nini kawafanyia Watanzania katika kipindi cha miaka mitano na kwanini anaomba tena kipindi kingine cha miaka mitano.
Miradi mikubwa ya miundombinu aliyotekeleza, mapambano ya rushwa na ufisadi, elimu bure, maboresho sekta ya afya na usimamizi wa rasilimali za Taifa kuwanufaisha wazawa ni baadhi ya vitu ambavyo vitambeba Rais Magufuli leo kuibuka na ushindi mkubwa.
Wakati wapinzani wake wakikosa cha kuahidi wananchi kutokana na kuwa tayari yeye alishaanzisha msingi wa karibu kila kitu, Rais Magufuli alijikita katika kueleza namna atakavyoendeleza miradi aliyoianzisha na kuendeleakusimamia rasilimali za watanzania.
Ni dhahiri kwamba upinzani mwaka huu walikwenda kwenye kampeni bila ajenda ya msingi kwani zilizokuwa ajenda zao za masuala ya rushwa na ufisadi pamoja na miundombinu mibovu ya huduma za kijamii vyote vimefanyiwa kazi ipasavyo katika serikali ya awamu ya tano.
KWANINI NI MAGUFULI LEO
JUNI 4, 2015 ndiyo siku safari ya Dk.John Magufuli ilipoanzia kuelekea Ikulu baada ya kufanya uamuzi wa kuchukua fomu ya kugombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), wakati huo akiwa ni Waziri wa Ujenzi.
Oktoba 29, 2015 baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, alitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC) kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais kwa kupata kura 8,882,935 ikiwa ni aslimia 58.46 huku mpinzani wake wa karibu Edward Lowassa wa chama cha Chadema akijipatia kura 6,072,848 ikiwa ni asilimia 39.97 ya kura zote.
Novemba 5, 2015 Dk. Magufuli alikula kiapo cha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuanza kazi hiyo rasmi akichukua nafasi ya Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete.
Wakati wa kampeni Rais Magufuli alitumia Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2015 ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kutangaza sera na ahadi za chama hicho.
Ahadi kubwa ambazo alikuwa akiziimba majukwaani mbele ya watanzania ilikuwa ni kutoa elimu bure, matibabu bure kwa watoto na wazee, alitangaza vita dhidi ya rushwa na ufisadi kwani aliweka wazi nia yake ya kuanzisha mahakama ya mafisadi, ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji, afya na elimu, kusimamia ipasavyo rasilimali za nchi ziwe na manufaa kwa wananchi wote na utawala bora.
Sasa ni miaka mitano imetimia akiwa ametekeleza kwa asilimia kubwa ilani ya uchaguzi yam waka 2015-2020 karibu katika kila sekta amefanya kitu kikubwa cha kuacha alama hata angeondoka leo madarakani.
MAPAMBANO YA RUSHWA
Rais Magufuli alieleza namna alivyotekeleza ahadi ya kupambana na rushwa na ufisadi ambapo alisema katika kipindi cha miaka mitano wamefanikiwa kupokea mashauri 407 katika mahakama ya rushwa na uhujumu uchumi iliyoanzishwa mwaka 2016.
Aliongeza kuwa kupitia Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mbali ya kufungua mashauri mbalimbali ya rushwa imefanikiwa katika kipindi cha miaka mitano kuokoa kiasi cha sh. Bilioni 273.38, zikiwemo fedha walizokuwa wamedhulumiwa wakulima.
Pia aliipongeza Mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya kwa kupunguza uingizaji wa dawa za kulevya kwa asilimia 90.
MAPATO
Rais Magufuli alisema katika kipindi cha miaka mitano wamejitahidi kuongeza uku- sanyaji wa mapato kwa kusi- mamia uadilifu kwa watumi- shi waliopewa dhamana ya kukusanya mapato, kuima- risha sheria za kodi, mifumo ya TEHAMA, kupanua wigo wa walipa kodi, kupunguza misamaha na kuziba mianya ya ukwepaji kodi.
Alisema kutokana n ajiti- hada hizo ukusanyaji wa mapato ya kodi kwa mwezi uliongezeka kutoka wastani wa sh. bilioni 850 mwaka 2015 hadi sh. trilioni 1.3.
Aliongeza kuwa walifani kiwa kuongeza pia ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi na yale ya halmashauri na kufanya mapato ya ndani kwa ujumla, kuongezeka kutoka sh trilioni 11.0 mwaka 2014/2015 hadi sh. trilioni 18.5 Mwaka wa Fedha 2018/2019.
Sambamba na kuongeza ukusanyaji wa mapato, Rais Magufuli alisema “tumedhibiti matumizi ya fedha za Serikali wa kuzuia au kupunguza safari za nje zisizo za lazima, semina, warsha, makongamano, matamasha na udanganyifu kwenye manunuzi.”
Alibainisha kuwa kutoka na na kuongezeka kwa mapato na kudhibiti matumizi, Serikali iliweza kuongeza bajeti ya maendeleo kutoka wastani wa asilimia 26 hadi asilimia 40.
HUDUMA ZA KIJAMII
Kwa upande wa huduma za jamii, Rais Magufuli alisema, “tumepanua wigo na kuboresha upatikanaji wa huduma za elimu, afya pamoja na maji.
“Kwenye elimu, kama unavyofahamu, tulianza kutoa elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari ambapo mpaka mwezi Februari 2020 tulikuwa tumetumia sh. trilioni 1.01 kugharamia.”
Alisema mbali na kutoa elimu bure pia wamefaniki wa kuongeza idadi ya shule za sekondari na msingi, kuongeza madawati, madarasa, vifaa vya maabara, ujenzi wa nyumba za walimu na ukarabati wa shule kongwe 73.
Alisema maboresho yote hayo yamesaidia kuongeza idadi ya uandikishaji wa fikia asilimia 94 mwezi Disemba 2019.
AFYA
Kwa upande wa sekta ya afya, Rais Mafufuli alisema wameongeza idadi ya vituo vya kutolea huduma za afya 1,769, zikiwemo zahanati 1,198, vituo vya afya 487, hospitali za wilaya 71, hospitali za mikoa 10, ikiwemo Hospitali ya Mkoa wa Mara, (Mwalimu Nyerere Memorial Hospital) ambayo ujenzi wake ulikwama tangu miaka ya 1970.
Mbali na hayo alisema waliweza kuongeza bajeti ya dawa na vifaa tiba, ununuzi wa mitambo ya kisasa na kusomesha wataalamu wa afya kuwa mabingwa na hivyo kupunguza idadi ya rufaa za wagonjwa kutibiwa nje ya nchi.
MAJI
Kuhusu maji, alisema wametekeleza miradi ya maji 1,423, ambapo miradi 1,268 ni ya vijijini na 155 ni ya mijini. Alitaja miongoni mwa miradi mikubwa inayoendelea kutekelezwa ni wa kutoa maji Ziwa Victoria kwenda Nzega, Tabora na Igunga;
Mradi wa Maji wa Arusha pamoja na mradi wa kupeleka maji kwenye miji 28 unaotekelezwa kwa gharama ya shilingi trilioni 1.2,” alisema Rais Magufuli.
“Kutokana na jitihada zilizofanyika, upatikanaji wa majisafi na salama vijijini umeongezeka kutoka asilimia 47 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 70.1 mwaka 2020; na kwa mijini kutoka asilimia 74 mwaka 2015 hadi asilimia 84 mwaka 2020,” alisema Rais Magufuli.
MAWASILIANO NA UCHUKUZI
Kwa upande wa huduma za mawasiliano Rais Magufuli alisema wameboresha usikivu wa simu kutoka asilimia 79 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 95.
Sambamba na hayo, alisema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, wamefanikiwa kufufua Shirika la Simu (TTCL) ambalo lilikuwa limekufa pamoja na kuongeza hisa kwenye Kampuni ya Airtel kutoka asilimia 40 hadi asilimia 49.
“Huu ni ushahidi mwing-ine kwamba kazi tuliyotumwa na Watanzania tumeifanya kikamilifu,” alisisitiza Rais Magufuli.
Alisema mbali na kuboresha huduma za jamii, wametekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hususan ka- tika ujenzi, uchukuzi na nishati ya umeme.
“Tumekamilisha ujenzi wa barabara zenye urefu wa takriban kilometa 3,500 na hivyo kuifanya nchi yetu iwe na kilometa 12,964 za barabara za lami.
Aliongeza kuwa barabara nyingine zenye urefu wa zaidi ya kilometa 2,000 zinaendelea kujengwa.
“Aidha, kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu, tumejenga barabara za juu (flyover na in- terchange) Dar es Salaam ili kupunguza tatizo la msongamano wa magari na pia tumekamilisha ujenzi wa madaraja makubwa 13,” alisema.
Alisisitiza, “Kwa ujumla, katika Awamu hii, hakuna Mkoa au Wilaya ambayo haikupatiwa fedha za kujenga barabara za lami. Makao Makuu ya Mikoa na Wilaya karibu zote sasa ya nameremeta kwa lami na taa za barabarani. Na ahadi yetu ya kuunganisha Mikoa kwa barabara za lami nayo imetekelezwa kwa asilimia kubwa,” alisema.
KUFUFUA USAFIRI WA RELI
Sambamba na kujenga barabara Rais Magufuli alise- ma wanakamilisha Awamu ya Kwanza ya ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro yenye urefu wa kilometa 300 na ujenzi wa Awamu ya Pili kutoka Morogoro hadi Makutupora umbali wa kilometa 422 umefikia asilimia 30, “Miradi hii miwili inagharimu shilingi trilioni 7.062.
“Ujenzi wa sehemu ya Mwanza Isaka – Dodoma ipo kwenye maandalizi. Tumekarabati pia reli ya zamani kutoka Dar es Sa- laam hadi Isaka kilometa 970 na halikadhalika tumefufua usafiri wa reli ya Dar es Salaam –Tanga – Moshi – Arusha, ambao ulisimama kwa takriban miaka 20,” alisema.
Kwa upande wa usafiri wa anga alisema wamejenga na kukarabati viwanja vya ndege vipatavyo 11 pamoja na kufufua Shirika la Ndege ATCL kwa kununu ndege mpya 11 na ambapo nane zimeshawasili tayari.
Ukiachilia mbali uimarishaji wa miundombinu ya usafiri, Rais alisema wameboresha upatikanaji wa nishati ya umeme kwa kujenga miradi ya kuzalisha umeme wa gesi na maji pamoja na ile ya kusambaza umeme.
Kutokana na jitihada hizo alisema wameongeza idadi ya vijiji vilivyofikishiwa umeme kutoka 2,018 mwaka 2015 hadi vijiji 9,112 mwezi Aprili 2020.
“Nchi yetu ina vijiji 12,268; hivyo tumebakisha vijiji 3,156 tu kufikisha umeme kwenye vijiji vyote nchini.”
Alisema moja ya ahadi zake ni kukuza sekta zetu kuu za uchumi na uzalishaji, ikiwemo viwanda, kilimo, biashara, madini pamoja na utalii.
“Kuhusu viwanda, tumejenga viwanda vipya 8,477, ambapo vikubwa ni 201, vya kati 460, vidogo 3,406, na vidogo sana 4,410,” alibainisha. Kuhusu kilimo ambacho kinachangia takriban asilimia 25 ya fedha za kigeni, asilimia 30 ya Pato la Taifa, asilimia 65 ya malighafi za viwandani, asilimia 70 ya ajira zote nchini na asilimia 100 ya mahitaji yetu ya chakula, alisema “tumeendelea kuipa kipaumbele sekta hiyo.”
“Tumeongeza upatikanaji wa pembejeo na zana za kili mo (mbegu bora, mbolea, viatilifu, matrekta), tumeongeza uzalishaji wa miche ya mazao ya kimkakati, tumejenga na kukarabati skimu za umwagiliaji, vihenge vya kuhifadhi mazao, tumetafuta masoko na kuviimarisha vyama vya ushirika.”
Alisema kutokana na hatua hizo, mafanikio makubwa yamepatikana.
“Mathalan, uzalishaji wa mazao ya chakula umeongezeka kutoka tani 15,528,820 mwaka 2015/2016 hadi tani 16, 891, 974 mwaka 2018/2019,” alisema.
Rais alisema mambo waliyofanya ni mengi na mafanikio ni makubwa, “nikisema nieleze hapa yote tunaweza kukesha.”