INSTABUL, UTURUKI
BAADA ya kutokea vitendo vya kibaguzi juzi na kuahirishwa mchezo kati ya Paris St-Germain dhidi ya Istanbul Basaksehir, mchezo huo uliamuriwa kurudiwa jana kuanzia dakika 14 uliposimamishwa.
Mchezo kati ya Paris St-Germain dhidi ya Istanbul Basaksehir utachezwa siku ya Jumatano baada ya kutelekezwa
Ikumbukwe mchezo huo ulivunjika siku ya juzi Jumanne wakati afisa wa mechi hiyo aliposhutumiwa kutoa maneno ya kibaguzi.
Instanbul ilidai mwamuzi wa nne Sebastian Coltescu alitumia lugha ya kibaguzi kwa kocha wao Msaidizi Pierre Webo.
Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa, Webo alioneshwa kadi nyekundu baada ya kurushiana maneno na muamuzi wa nne
Wachezaji wa Instambul walitoka nje ya uwanja wakikemea kitendo hicho, huku PSG wakifuatia
Tukio hilo lilitokea dakika 14 tu tangu kuanza kwa mchezo wa kundi H, mchezo ambao walikuwa hawajafungana.
Mchezo huo ulipangwa kuanzia dakika ya 14 uliposimama juzi Jumanne, mchezo ulipangwa kuanza saa 2:55 saa za Afrika Mashariki.
Maafisa wengine waliotarajiwa kuusimamia mchezo huo, walikuwa Mholanzi Danny Makkelie akiteuliwa kuwa mwamuzi.