Ubadhirifu miradi ya serikali, uimara wa majengo kuchunguzwa

0

Serikali ya mkoa wa Kaskazini Unguja imeunda timu ndogo ya uchunguzi ya wataalam itakayoongozwa na mamlaka ya majengo ya Serikali kuchunguza uimara wa jengo la huduma za Mama na mtoto liliopo kivunge Wilaya ya Kaskazini A.

Hatua yakuundwa timu hiyo ya wataalamu ni baada yakuibuka taarifa za jengo hilo kuanza kubomoka, ambapo serikali ya mkoa wa kaskazini imefika katika hospitali hiyo na kubaini kilichotokea ni kubanduka kwa plasta ya juu na sikuta za jengo hilo kama ilivyoripotiwa awali.

Kwenye ukaguzi wa awali kilichobainika ni kuanguka kwa dari ya chumba cha huduma za watoto.

Na hali hii inatokea ikiwa ni takribani siku sitini zimepita toka rais mstaafu wa awamu ya saba Dkt. Ali Muhammedi Shein alipolizindua rasmi jengo hilo mnamo oktoba 13, 2020.

Kazi nyingine ya kamati ya uchunguzi itatoa ushauri wa nini kifanyike kwenye taarifa yao.

Mkurugenzi wa wakala wa majengo Zanzibar, Ramadhan Mussa Bakari, amesema timu hiyo ya uchunguzi itasimamia ukweli na uwazi kwa kile watachokibaini, huku mhandis mkuu wa wizara ya afya, Talha Masoud amesema kwa upande wa kitaalamu hilo ni jambo la kawaida.

Jengo hili lililobanduka dari, kuta nazo zimeanza nyufa na baadhi ya vyoo kuvujisha maji lakini.

Kwa mujibu wa mhandisi mkuu wa Wizara ya Afya jengo hilo lililowekwa jiwe la msingi na makamu wa rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Januari 9, 2020,na kuzinduliwa rasmi tarehe 13/10 2020 na rais mstafu awamu ya saba Dk. Ali Mohammed Shein lipo chini ya uwangalizi wa miezi mitano na ikitokea kasoro mkandarasi aweze kurekebisha kasoro hizo.

Dk. Shein alipozindua jengo la Mama na Mtoto katika hospitali ya Wilaya Kivunge, Mkoa wa Kaskazini Unguja, oktoba 13, 2020

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here