Tuzingatie tahadhari ya TMA kuhusu mvua kubwa mikoa sita

0

MARA nyingi zinaponyesha mvua kubwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini kumewawapo na madhara ambayo ynaweza kuepukwa endapo wananchi watachukua tahadhari zinazotolewa na mamlaka husika.

Miongoni mwa athari zinazotokea panapokuwa na mvua kubwa ni pamoja na watu kupoteza maisha, mali kuzolewa na maji na nyumba kujaa maji. Licha ya kwamba baadhi ya athari hizi hazikwepeki kama vile nyumba kujaa maji lakini taarifa za mamlaka zikizingatiwa wananchi wanaweza kuepuka athari nyingine kama vifo na mali kusomwa maji.

Jana Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mvua kubwa  zinatarajiwa kunyesha  kwa siku mbili katika mikoa sita  na kuleta athari katika mikoa hiyo.

Mikoa inayotarajiwa kunyesha mvua hizo ni Iringa, Njombe, Lindi Mtwara, Ruvuma na Morogoro.

Taarifa ya TMA iliyotolewa imesema mvua hizo zinatarajiwa kunyesha juu ya wastani kuanzia jana hadi Desemba 27,  2020.

Imesema zinaweza kusababisha  mafuriko na barabara kutopitika na baadhi ya makazi ya watu kuzungukwa na maji na kuwataka wananchi kuchukua tahadhali.

Pia,  TMA imetoa  tahadhali ya kuwepo kwa mawimbi makubwa yanayofikia ukubwa wa mita 2.0 na upepo unaokwenda kasi kilometa 40 kwa saa utakaosababisha kuathiri shughuli za uvuvi, usafiri baharini na upatikanaji wa samaki.

Imesema upepo huo unatarajiwa kuanza Desemba 28, 2020 maeneo ya Pwani ya bahari ya Hindi katika mikoa ya Lindi,  Mtwara, Dar es Salaam, Pwani, Tanga,  Mafia, Unguja na Pemba.

TMA imewashauri watumiaji wa bahari ya Hindi wachukue tahadhali na hatua stahiki huku wakiendelea kufuatilia hali hiyo a watatoa mrejeo kila itakapobidi.

Sisi Jamvi la Habari tunaungana na TMA kuwasihi wananchi wa mikoa iliyotajwa kuzingatia tahadhari hiyo badala ya kupuuza na kujikuta katika matatizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here