TUTAZIDI KUIMARISHA MUUNGANO- MAGUFULI

0

WA N A N C H I pamoja na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar wameudhihirishia umma kuwa chama hicho bado kipo imara visiwani Zanzibar mbali ya maneno ya upinzani kutaka kuuaminisha umma kuwa kimepoteza mvuto. Hayo yamedhihirika jana katika viwanja vya Mazi Mmoja kutokana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza kusikiliza sera za wagombea urais kwa pande zote za muungano Dk. John Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dk. Hussein Mwinyi kwa upande wa Zanzibar.

Dk. Magufuli alionyesha kuvutiwa na idadi kubwa ya watu walioanza kukusanyika saa moja asubuhi wakati mkutano ulitakiwa kuanza mchana, hii ni dhahiri watu walikuwa na kiu ya kutaka kumsikiliza na kumuona mgombea wao ambaye ndani ya miaka mitano ya uongozi wake alifanya mambo makubwa kimaendeleo. Alisema, “Huu umati uliojitokeza sijawahi kuuona tangu nilipoanza mbio zangu za kampoeni, hongereni Wazanzibari na kwa heshima mliyonipa nimebaki na deni kubwa la kiwafanyia kazi. Inadhihirisha Zanzibar mwaka huu mmeamua.”

Akizungumzia historia ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1964, Dk. Magufuli alisema kuundwa kwa taifa la Tanzania kumekuwa gumzo duniani kwa kuwa wakoloni hawakutaraji kuona taifa la kiafrika linaungana na kudumu kwa miaka mingi sasa bila kutetereka. “Mataifa ya Ulaya yalikutana Berlin ili kuigawa Afrika, machungu ya kutawaliwa tunayajua. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni wa kipekee taifa lililoundwa na wazalendo chini ya Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume.“Huu ni muunganiko wa kidugu na kisiasa kwa kuinganisha ardhi na vyama vya siasa AfroShirazi Party na TANU.

Ukisikia mtu anasema muungano huu ni wa kulazimishwa ujue huyo ni mzushi. Tumepata taifa lenye uhuru wa kweli tumedhihirisha hilo wakati wa vita ya Kagera tulipovamiwa na Nduli Amin wa Uganda, tulisimama pamoja,” alisema Dk. Magufuli na kuongeza: “Hata wakati wa Corona tulikataa kupokea maelekezo ya kukaa ndani tulidhihirisha uhuru wetu, tuliamua tunakwenda kivyetu na leo corona haipo hapa.” Aidha, juzi alipowasili Dk. Magufuli alipata wasaa wa kuzungukia maeneo mbalimbali ikiwemo Hospitali ya Mnazi Mmoja pamoja na kuzungumza na wananchi waliofurika kumlaki Uwanja wa Ndege wa Abeid Karume visiwani humo.

Kwa upande wake Dk. Mwinyi alisema wapo watu wanaobeza juhudi kubwa inayofanywa na CCM katika kuimarisha muungano hata wakafikia hatua ya kudai ipo nia ya kuunda muungano wa nchi moja kitu ambacho si kwel. “Katika kampeni zetu hatuzungumzi mipasho bali tunaeleza sera za kimaendeleo, tunzungumzia uchumi wa Blue ambao utagusia maendeleo yatokanayo na bahari hasa uvuvi, wapinzani wetu hawajui chochote maana wanasema upande wa pili wa muungano utatuzuia kuvua kitu ambacho si kweli kwa kuwa mamlaka ya uvuvi makao makuu yake yapo Zanzibar. “Upo utaratibu uliowekwa ambapo mapato yatokanayo na uvuvi kwanza mamlaka itapata asilimia 50 kisha asilimia 30 itakwenda Tanzania Bara na asilimia 20 itakuwa Zanzibar,” alisema Dk. Mwinyi.

Alipozungumzia suala la mafuta na gesi, alisema wapo wanaopotosha kuwa hata suala la mafuta halitakuwa na utaratibu mzuri wa kuinufaisha Zanzibar, lakini ukweli unajulikina. Akijibu suala hilo Dk. Magufuli alisema: Mafanikio makubwa yamepatikana tangu mwaka 1964 tumeingia katika uchumi wa kati hii ni kwa sababu ya muungano. Wapo wanaosema mapato hayalingani katika migawanyo. Miaka 40 zimekopwa fedha trilioni 2.3 kwa ajili ya znz kutoka Tanzania Bara. Umeme,barabara,kilimo,kiwanda cha sukari cha Mahonda nyumba za nafuu,afya,elimu,barabara za vijijini,maendeleo,kuondoa umaskini,maji,airporr terminal 2.

Miradi hii 1980 hadi 2020 sijataja ile ya nyuma na inayoendelea. Amekuza 2.4 hadi 3.1 trilioni amekuza uchimi kuanzia 2015. Makusanyo ya mapato bil 428.5 hadi bil 748.9 mfymulo wa bei 5.7 hadi 2.7 kukuza uchumi kwa asilimia 7. Amekuza selta ya utalio 294 elf hadi 538elf hivyo kuvuka lengo la ilani kwa mwala 2015. Sekta ya kilimo kwa kuongeza uzalishaki karafuu kutoka tani 3321 hadi tani 8277 na mpunga kutoka tani 281 hadi 276. Ole Kengeja barabara ameimarisha huduma za usafiri kwa kununua meli mpya MV Mapinduzi 2 na kukarabati mv maendeleo na mv mkombozi.

Shule za msingi 260 hadi 381 zimeongezeka nyingine za gorofa. Amejenga eneo la Malangale shule maalum za sayansi hisabati na fizikia. Amechimba visima 150 vya maji. Kuna wagombea hawana nia njema wanafanya mambo kama walivyoelelezwa na mabeberu kwa kutugawa vipande ili waibe mali zetu wakataeni watu hao. Nafahamu muungano una changamoto ndogo ndogo tutazimaliz biln22.9 zeco ilipodaiwa na tanesco nilizifuta kwa kuwa znz ni tz na tz ni znz. Sikutaka kuwatwisha mzigo waznz.

Mwinyi amekuwa waziri kwa miaka 20 nami nilikuwa waziri miaka 20 hii inamtosha kuwa rais wa znz. Amekuwa waziri wa ulinzi miaka 11 mizinga vifaru mabomu yote yanamjua hakuwa hata na tamaa ya kupindua nchi ana moyo wa pekee wenye uvumilivu. Alikuwa naibu afya miaka mitano na mkapa alikuwa muungano miaka miwili akawa waziri wa ulinzi nikamchagua pia. Ubaya wenu baadhi yenu waznz wazuri hamuwajui. Pemba alikuwepo Prf Mbarawa hawakumtaka nikampa uwaziri wa brbr nikampeleka maji akaongoza vzr lkn Pemba hawamjui kama ni dhahabu. Utamlinganisha Mwinyi na waliogombea miala 25 uligombea na babu na sasa wajukuu.

Znz inataka maendeleo na kama mnayataka chagueni Dk. Mwinyi. Nakuomba utakapochaguliwa kuwa rais hakikisha makamo wako wa pili wa rais anatoka Pemba. Unguja na Pemba mgawanyiko unatakiwa upotee. Hili ni taifa moja. Tangu muungano viongozi wengi ni wale waliozaliwa kabla ya muungano sasa tunataka aliyezaliwa baada asilimia 70 waznz wamezaliwa baada ya muungano anajua hitaji kubwa la waznz. Wanataka kuona fursa za kiuchumi na biashara zinaendelezwa. Najua kuna suala la mafuta. Mafuta yatakayopatikana huku ni ya waznz kama sisi tulipata dhahabu ni yetu.

Mnahitaji mtu atakayeyasimamia mafuta yawaendeleze. Atayasimamia kwa maslahi ya waznz. Pia hapendi rushwa uzembe dhuluma. Wakinamama wajane wanadhulumiwa tunahitaji mtu kama mwinyi akasikilize matatizo yake. Sura ya 1,8 na 9 zote zimezungumzia suala la muungano katika ilani ya ccm. Nitashirikiana naye kuleta mapinduzi ya uchumi. Tuna maeneo mengi ya kushirikiana uchumi wa bahari biashara na utalii kilimo na ujenzi wa miundombinu. Kuna vikwazo vidogo vya wafanyabisahara tutavitatua tutaifanya znz kuwa kituo cha biashara sisi ni wamoja na lengo letu ni kuifanya nchi kuwa nzuri.

Nilikuwa waziri wa uvuvi deep sea authorotu nilipeleka mm bungeni makao makyu ya uvuvi yapo znz nani anasema watakatazwa. Ni wachonganishi hili ni taifa moja hata meli za uvuvi zinasajiliwa hapa hili wanatakiwa walalamike tz bara. Zitanunuliwa meli 8 za uvuvi kila eneo nne. Tumeupanua uwanja wa ndege. Na yale aliyoyaomba mgombea tutayatekeleza kwa pamoja. Mwinyi wakati mwingine pia ni mkali ndio nampendea. Mwinyi anatosha mtayaona mafanikio yake wanaompiga vita ni kwa sababu hawataki nyinyi mfanikiwe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here