Na Mwandishi Wetu
Siku chache baada ya kuomba hifadhi katika ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania aliyekuwa mgombea urais wa Chadema, Tundu Lissu amesema leo Jumanne Novemba 10, 2020 ameondoka kwenda Ubeligiji alikokuwa akiishi tangu Januari 2018.
Lissu aliyeomba hifadhi katika ubalozi wa Ujerumani tangu Novemba 2, 2020 akidai kutishiwa maisha yake, amesema anasafiri kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia itakayopitia Addis Ababa, kisha Vienna Austria na kituo cha mwisho kitakuwa Brussels, Ubeligiji.
“Nakwenda Ubelgiji. Sio political asylum (hifadhi ya kisasa), mimi nina ruhusa ya kukaa Ubelgiji tangu nilipokwenda kwa matibabu Januari 2018. Kwa hiyo sihitaji kuomba political asylum,” amesema na Lissu na kuongeza kuwa;
“Sikimbii mapambano, ila nakwenda uwanja mwingine mpya wa kudai haki, demokrasia na utu wetu kwa nchi yetu.”