Tumetekeleza Ilani kwa asilimia 99.9-Samia

0
Samia Suluhu Hassan akihutubia Mkutano wa kampeni za CCM katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Paje Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja

 NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR

MGOMBEA mwenza wa kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu Hassan, alisema CCM imetekeleza ilani ya uchaguzi  ya mwaka 2015/2020 kwa asilimia 99.9.

Alisema maendeleo hayo yaliyofikiwa ni kutokana na usimamizi mzuri wa sera za Serikali zote mbili zilizopo chini ya CCM.

Alisema CCM iliyotokana na vyama viwili vya ukombozi ambavyo ni TANU na ASP ambavyo vilizaa chama chenye nguvu na kinachojali maendeleo ya watu wa makundi yote.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kampeni za kuwaombea kura wagombea wa CCM huko Paje Wilaya ya Kusini Unguja,alisema wananchi wanatakiwa kuwachagua wagombea wa CCM ili nchi iendelee kupaa kiuchumi.

Alisema kuichagua CCM ndio ishara ya kudumu ya kulinda tunu za muungano,Mapinfuzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 na uhuru wa nchi.

Alisema CCM itaendea kuenzi utawala bora kwa maendeleo endelevu ya nchi.

Alielezea historia ya muungano kwa kueleza kwamba vyama vya upinzani havina nia njema na maendeleo ya nchi kwani nia yao ni kuvunja muungano.

Aliwaomba wananchi wawakatae na kutowachagua wanasiasa wenye nia ya kuvunja muungano hawafai kupewa nchi kwani ni madalali wa kisiasa.

Akitaja sifa za mgombea urais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi,kuwa ni mtu mstaarabu na mwenye uzoefu mkubwa kiungozi.

Mgombea huyo mwenza wa kiti cha urais wa muungano Samia, alisema mgombea urais wa jamhuri ya muungano Dkt.Magufuli ni kiongozi makini na mwenye nia ya kweli ya kuleta maendeleo ya nchi.

Katika maelezo yake mama samia alisema serikali zote mbili zimejipanga vizuri kulinda amani ya nchi wakati wote wa uchaguzi.

Alisema vipo viashiria vya uvunjifu wa amani vinavyofanywa na baadhi ya vyama vya upinzani kwani wanajua kuwa CCM itashinda kwa asilimia kwa kiwango cha juu.

Katika mkutano huo aliwaombea kura wagombea wote wa CCM wakiwemo mgombea urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM  Dk.John Pombe Magufuli,mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk.Hussein Ali Mwinyi,wabunge,wawakilishi na madiwani wa CCM.

Alieleza kwamba katika vipaumbele vya mgombea amesema atajenga bandari ya kisasa ya kizimkazi, hivyo na yeye amesema ataunga mkono ujenzi huo ili wananchi wapate ajira.

Kwa upande wa mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk.Hussein Ali Mwinyi,alisema atajenga bandari ya kisasa ya Kizimkazi ili wananchi wa maeneo hayo na maeneo jirani wapate ajira.

Alisema kuna baadhi ya wanasiasa wanadai kuwa Zanzibar haiwezi kujenga bandari ya kisiasa kwani haitopata mkopo Jambo ambalo sio sahihi kwani tayari serikali ya muungano ipo tayari kutoa ushirikiano.

Alisema kuwa suala la mafuta na gesi lishaondolewa katika masuala ya muungano na Zanzibar inayo sheria yake ya kumiliki rasilimali hiyo.

Alisema atawekeza kwenye miundombinu ya elimu kwa kujenga na kukarabati shule mbalimbali ndani ya wilaya hiyo  ili kumaliza changamoto ya upungufu wa shule na vifaa vya kisasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here