Trump apinga mpango wa kuwapa chanjo ya corona maafisa wa Ikulu

0

NEWYORK,MAREKANI


RAIS wa Marekani Donald Trump amebadili mpango wa kuwapa chanjo ya corona maofisa wa White House katika siku chache zijazo.

Awali maofisa walisema maafisa wa ngazi ya juu katika utawala wa Trump watakuwa miongoni mwa watu wa kwanza kupewa chanjo ya corona, maafisa nchini Marekani wamesema.

Maafisa pia walikuwa wamesema baadhi ya wafanyakazi wa White House wanatarajiwa kupewa chanjo ya Pfizer/BioNTech wiki hii.

Chanjo hiyo inatoa ulinzi wa hadi asilimia 95 dhidi ya Covid-19 ana inaidhinishwa kuwa salama na wadhibiti wa dawa wa Marekani iliyopita Ijumaa.

Dozi milioni tatu za kwanza za chanjo hiyo kwasaba zinasambazwa katika maeneo tofauti katika majimbo yote 50 ya Marekani.

Shehena ya kwanza ya dozi hizo iliwasilishwa Michigan siku ya Jumapili, wahudumu wa afya na wazee ndia wanaotarajiwa kupewa mapema Jumatatu.

Vifo vilivyotokana na corona vimeongezeka sana mwezi Novemba nchini Marekani, ikivunja rekodi duniani kwa kuwa na idadi ya juu zaidi ya maambukizi ya 3,309 siku ya Jumamosi.

Lakini kuzinduliwa kwa mpango wa chanjo kunachukuliwa kuwa hatua kubwa katika mapambano dhidi

Mamlaka ya chakula na dawa (FDA) imesema kuwa imeamua kuidhinishwa chanjo ya dharura, katika tangazo lake la Ijumaa kama “hatua muhimu” katika jitihada za kukabiliana janga la corona, baada ya utawala wa Marekani kushinikizwa vikali kuidhinisha chanjo hiyo.

Mpango wa kutoa chango kama hiyo unaendelea nchini Uingereza. Chanjo ya Pfizer pia imeidhinishwa nchini Canada, Bahrain na Saudi Arabia.

Baadhi ya chanjo za kwanza zimetengewa watu waliofanya kazi kwa karibu na Bwana.Trump, mafisa wameambia vyombo kadhaa vya habari nchini Marekani.

Lakini baadae chanjo hiyo itapewa maofisa wa vitengo vitatu vya serikali, ikiwa ni pamoja na White House, Congress na Mahakama ya Juu Zaidi.

Afisa mmoja ambaye jinalake halikutajwa ameambia Shirika la Habari la Reuters kwamba chanjo itahakikisha serikali inaweza “kuendelea na kutekeleza shughuli zake muhimu, bila

Mkuu wa wahudumu wa White House Mark Meadows ni miongoni mwa watu wa karibu na Rais Trump ambao waliambukizwa Covid-19

Mpango huo wa chanjo ambao kwanza uliripotiwa mara ya kwanza na Gazeti la New yORK Times, umethibitishwa na msemaji wa Baraza la Kitaifa ya Usalama (NSC) John Ullyot siku ya Jumapili.

Lengo kuu la mpango huo ni kujenga imani ya umma kuhusu chanjo hiyo, alisema.

“Watu wa Marekani waamini kuwa wanapokea chanjo salama na inayofanya kazi ambayo piwa imepewa maofisa wa ngazi ya juu wa serikali ya Marekani kutokana na ushauri wa waataalamu wa afya ya umma na uongozi wa usalama wa kitaifa,” Bw. Ullyot alisema.

Baadaye Jumapili Rais Trump alifafanua katika Twitter yake kwamba “watu wanaofanya kazi White House watapokea chanjo hiyo baadaye katika mpango huo pengine iwe lazima”.

Bw Trump, ambaye aliyeambukizwa virusi vya corona mwezi Novemba na kupona baada ya kutibiwa hospitalini, aliongeza : “Mimi sijapangiwa kupewa chanjo hiyo lakini natazamia kupewa wakati kwafaka ukiwadia.”

Kumekuwa na visa kadhaa vya mlipuko wa virusi vya corona katika Ikulu ya White House, huku maofisa kadhaa wa ngazi ya juu wakiripotiwa kupatikana na maambukizi ya ugonjwa huo.

Haijabainika, ikiwa Naibu wa Rais Mteule Kamala Harris na wanachama wa kundi lake watapewa chanjo hiyo ya mapema.

Pfizer/BioNtech ni kampuni ya kwanza ya dawa kutoa maelezo kuhusu awamu ya mwisho ya kufanyia majaribio chanjo yake.

Ni aina mpya inayoitwa mRNA inayotumia alama za chembechembe za jeni ya urithi kutoka kwa virusi kuufundisha mwili jinsi ya kupamabana na Covid-19 na kujenga kinga ya mwili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here