TRUMP APATA CORONA

0

Trump na mke wake wamepatikana na virusi vya corona na sasa wako kwenye karantini.

Rais Donald Trump wa Marekani amesema kwamba yeye na mke wake Melania Trump wamepatikana na virusi vya corona na wako kwenye karantini.

Bwana Trump, 74, na hivyo basi yuko katika kundi lililo kwenye hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa huo, ameandika kwenye mtandoa wa Twitter: “Tutapita hili pamoja.”

Ametoa tangazo hilo kwenye mtandao wa Twitter.

Tangazo hilo linawadia baada ya Bwana Trump na wasaidizi wake wawili kuthibitishwa kuambukizwa virusi vya corona.

Aidha awali mke wa rais Melania Trump alituma ujumbe kuashiria kwamba wanaendelea vizuri.

”Kama ambavyo raia wengi wa Marekani wamefanya mwaka huu, Rais Trump na mimi tuko kwenye karantini nyumbani baada ya kuthibitishwa kuwa na virusi vya corona. Tunaendelea vizuri na nimeahirisha shughuli zote zijazo. Tafadhali hakikisha uko salama na tutashinda changamoto hii pamoja.”

Hope Hicks, 31, mshauri wa rais amekuwa msaidizi wa karibu wa Bwana Trump kupatikana na virusi vya corona hadi hivi sasa.

Bi. Hicks alisafiri na Bwana Trump kwa ndege ya kijeshi kwenda kwenye mdahalo wa Televisheni alipokabiliana na mpinzani wake Joe Biden Jumanne.

Mapema Alhamisi, Bwana Trump alisema yeye na mke wake, 50, wanakwenda karantini baada ya Bi. Hicks kuthibitishwa kuwa na corona.

Ameandika kwenye mtandao wa Twitter: “Hope Hicks, ambaye amekuwa akifanyakazi kwa bidii sana bila hata kupumzika, amethibitishwa kuambukizwa ugonjwa wa Covid-19.

“Mke wangu na mimi tunasubiri matokeo yetu. Wakati huohuo, tutaanza mchakato wa kuwa kwenye karantini!”

Bado haijafahamika vile kuthibitishwa kwa Bwana Trump kutaathiri maandalizi ya mdahalo wa pili wa urais, ambao umepagwa kufanyika Oktoba 15 huko Miami, Florida.
Coronavirus.

Bwana Trump mara nyingi huwa havai barakoa na amekuwa akipigwa picha akiwa hazingatii hatua ya kutokaribiana akiwa na wasaidizi wake au watu wengine wakati wa ziara zake rasmi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here