Home HABARI Trump atangaza mkutano wa G7, kufanyika kwa njia ya mtandao kuepuka Corona

Trump atangaza mkutano wa G7, kufanyika kwa njia ya mtandao kuepuka Corona

Washington, MAREKANI

Rais wa Marekani, Donald Trump, amefuta Mkutano wa viongozi wa mataifa saba tajiri dunaini (G7), badala yake mkutano huo utafanya kwa njia ya video kutoa fursa kwa viongozi kushughulikia mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona katika nchi zao.

Mkutano huo uliokuwa uwakutanishe viongozi wa mataifa ya Canada, Ufaransa, Ujerumani, Japan, Italia, Uingereza na Marekani ulikuwa ufanyike mnamo Juni mwaka huu katika eneo la Camp David lililopo jimbo la Maryland nchini Marekani.

Trump pia atazungumza na viongozi wa mataifa hayo saba kwa njia ya video mnamo mwezi Aprili na Mei baada ya viongozi hao kufanya mkutano kuhusu mlipuko wa virusi vya corona wiki hii.

Kwa hali inavyoendelea, serikali ya Trump inaamini mlipuko wa virusi vya corona utaendelea kuwa na athari ulimwenguni hadi majira ya joto.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -

Most Popular

Yanga yampatia Tshishimbi mkataba mpya

NA MWANDISHI WETU Klabu ya Yanga SC, imesema kuwa tayari imemaliza kazi yake ya kuhakikisha inambakiza kiungo tegemeo wa...

Tetesi za soka barani Ulaya

SANCHO AITIKISA UNITED Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Timu ya Taifa ya Uingereza, Jadon Sancho (20), amesema hatakuwa tayari...

Makonda: Wazururaji hawatakwenda mahabusu watazibua mitaro ya maji machafu

NA MWANDISHI WETU Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema kuwa watu watakaokamatwa kwenye mkoa huo kutokana...

Chui katika hifadhi ya wanyama ya Bronx akutwa na Virusi vya Corona

NEW YORK, MAREKANI Chui wa kike wa Malaysia aliyefahamika kwa jina la Nadia mwenye umri wa miaka minne katika hifadhi...

Recent Comments