TPA YAKABIDHIWA GATI JIPYA: WAZIRI AAGIZA UCHIMBAJI WA KINA UFANYIKE KWA MIEZI 18 BADALA YA 30.

0

*YAKABIDHIWA GATI NAMBA 5,
*WAZIRI AAGIZA UCHIMBAJI WA KINA UFANYIKE KWA MIEZI 18 BADALA YA 30.
*KUHUDUMIA SHEHENA TANI MILIONI 20 MWAKA 2022.

Na Merciful Munuo
Waziri wa Uchukuzi Dk Leonard Chamuriho amemtaka Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Uchimbaji wa kina cha Bandari ya Dar es Salaam, kutekeleza Mradi huo kwa Muda wa Miezi 18, tofauti na Mkataba ulioelekeza Mradi huo utekelezwe kwa muda wa siku 30.

“Mkandarasi huyu ameonyesha uwezo Mzuri wa Uchimbaji wa kina cha Bandari ya Tanga, kwahiyo kwenye Mradi huu naagiza autekeleze kwa muda wa miezi 18 kwasababu uwezo anao” Alieleza Waziri.

Aidha Dk Chamuriho ameyasema hayokabidhiwa Gati Namba 5 la Bandari ya dar es Salaam na Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, huku akiendelea na Ujenzi wa Magati Mengine.

Waziri Chamuriho pia ameelekeza utekelezaji wa ujenzi wa Magati mawili ya Namba 6 na Namba 7 yatekelezwe kwa Wakati, pamoja na Mradi wa Kuingiza Reli ya SGR kwa Wakati ili ziweze kutoa huduma ikiwemo kuhamishia Maksha ya Makontena Kwenye bandari Kavu ya Kwala.

Aidha Mkurugenzi Mkuu wa Bandari akitoa taarifa ya Ujenzi wa gati Hilo ameeleza kuwa katika Programu za utekelezaji wa Mradi wa Upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Na Hivyo Kufanya Bandari Hiyo kuwa Na magati 6 yaliyopo Tayari na ambayo yanaweza kufanya kazi Ipasavyo.

“Gati Namba 6 Ujenzi umefikia asilimia 96 na Ujenzi Namba 7 ambayo yenyewe imekamilika kwa asilimia 70 mpaka kukamilika ambapo kutoka Gati namba 5, 6, na 7 ni Mahali patakapotumika kwaajili ya kuhudumia shehena za makasha, ambapo tumekubaliana na Mkandarasi na atamaliza sehemu kubwa mwezi wa 6, ili ikifika mwezi wa 7 tutaanza “kuyatumia Magati haya” Aliongeza Mkurugenzi Kakoko.

Aidha Kakoko alieleza kuwa Bandari iliendelea kutekeleza Miradi hiyo hata Kipindi ambapo kulikuwa na msukumo wa Virusi vya Korona jambo llilopelekea kufikia hatua kubwa ya Ujenzi wa Miradi Hiyo pamoja na Ukusanyaji wa Mapato.

“Tulikusudia kufikia Tani Milioni 18, lakini Mpaka Tulipofika Decemba tuliweza Kupata tani Milioni 400, Lakini Tani Zilipungua Baada ya Kushuka kwa Bei ya Mafuta, hivyo Ongezeko letu la Shehena zilifikia Tani Milioni 17.5, huku wenzetu wakishuka zaidi na baadhi ya shehena zao kuanzankuletwa kwenye bandari zetu” Alieleza Kakoko

Mkurugenzi Kakoko pia amemwomba Waziri kuwa bandari ipewe Kipande Chote cha Maji kilichoingia kwenye eneo la ardhi ili waweze kujenga Magati na kutoa kwa makampuni makubwa ya usafirishaji wa shehena ili kuongeza idadi ya shehena TPA inazohudumia.

Aidha Baada ya kukamilika kwa Maboresh yanayoendelea TPA inatarajia kukusanya Shehena Tani Milioni 25, ambapo kufikia mwaka 2022 inatarajia kufikia Tani Milioni 20.

Aidha Kukamilika Kwa Mradi huo pia Kutawezesha Bandari kuweza kuhudumia Makasha Mengi kulko yale yanayohudumiwa na TICS ambapo Meli zitakuwa zikiiingia moja kwa moja bila kukaa kusubiri foleni hivyo kupunguza Muda wa kupokea shehena

Hapo awali TPA Ilikuwa ikihudumia Makontena Laki 2, Huku TICS wao wakihudumia Jumla ya makontena laki 5, ambapo baada ya kukamilika kwa Mradi huu sasa TPA itakuwa na Uwezo wa Kuhudumia hadi Makontena Laki 7 ambayo ni zaidi ya yale ya TICS.

Aidha TPA pia tayari imeshatenga maeneo kwaajili ya TBS ambapo sasa wanasubiriwa ili waweze kwenda kwenye eneo hilo la kukagulia nyaraka.

TPA pia ietenga eneo ambalo kutakuwa na Meli za Utalii, ambapo TPA inashirikiana na Wadau Mbalimbali ikiwemo eneo la bagamoyo ambapo Mwanzoni mwa mwaka 2022 wanatarajia wataanza ujenzi wa Gati la uvuvi.

Aidha Serikali pia Imeboresha FLOMITA ya uingizaji wa mafuta ambapo kwa sasa itakuwa na uwezo wa kuhudumia shehena za Mafuta kwa ufanisi zaidi kuliko hali ilivyokluwa hapo awali

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here