TP Mazembe wamtoa kwa mkopo Singano

0

NA MWANDISHI WETU

MCHEZAJI wa zamani wa Simba SC na Azam FC, Mtanzania Ramadhani Singano, ametolewa kwa mkopo wa mwaka mmoja kwenda Nkana FC ya Zambia akitokea TP Mazembe ya Congo DR.Singano alijiunga na TP Mazembe pamoja na Eliud Ambokile lakini uwepo wa wachezaji mahiri lukuki katika club ya TP Mazembe kumemfanya kukosa nafasi ya kucheza.

TP Mazembe inaarifiwa kuwatoa kwa mkopo Singano na Isaac Amoah kwenda Nkana FC ili wapate muda wa kucheza na kuboresha viwango vyao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here