TMA yatoa tahadhari mvua kubwa mikoa 6

0

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya uwepo wa mvua kubwa kwa siku mbili kuanzia jana Desemba 26 hadi 27 mwaka huu kwa mikoa sita huku pia kukitarajiwa  kuwepo na upepo mkali Desemba 28, 2020 kwa baadhi ya mikoa.

“Mvua hiyo yenye uwezekano wa wastani, itanyesha kwenye baadhi ya maeneo ya mikoa ya Iringa , Njombe, Lindi za Mtwara, Ruvuma pamoja na maeneo ya Kusini mwa Mkoa wa Morogoro.”

Kwa mujibu wa taarifa ya TMA iliyotolewa jana ilieleza  kwamba jana Desemba 26 na 27 mvua kubwa itanyesha kwenye baadhi ya mikoa hiyo.

“Athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji jambo linaloweza kuathiri shughuli za kiuchumi na ucheleweshwaji wa usafiri. Hata hivyo, TMA imewataka wananchi kuzingatia angalizo hilo.

Aidha taarifa hiyo imetoa angalizo la kuwepo kwa upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2.0 Desemba 28, mwaka huu.

 Angalizo hilo limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa Pwani  ya Bahari ya Hindi, (mikoa ya Lindi, Mtwara,  Tanga, Dar es Salaam, na Pwani ikijumuisha visiwa vya unguja na Pemba.

“Athari zinazoweza kujitokeza ni pamoja na kuathirika kwa shughuli za uvuvi na ucheleweshwaji wa usafiri

Taarifa hiyo inayoelezea hali ya hewa kwa siku nne kuanzia Desemba 26 imeonesha kuwepo kwa hali ya kawaida ya hewa kwa siku ya Desemba 29, 2020.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here