Tiketi ya Lissu kwenda Ulaya hii hapa

0

Ná Mwandishi Wetu

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Tundu Lissu amethibitisha kuwa, ni kweli ana tiketi ya ndege ya kuondoka nchini Desemba 18, 2020 kwenda Ubelgiji

Hata hivyo Lissu alijitetea kuwa ataenda kutokana na matatizo ya kiafya aliyoyapata baada ya kupigwa risasi mwaka 2017, ambapo daktari wake amemuambia Desemba 20 arudi Ubelgiji ili aangalie maendeleo yake

Lissu alisema hayo akimjibu Mgombea wa Urais kupitia CCM, Dk. John Magufuli ambaye alisema ana taarifa kuna baadhi ya wagombea wana tiketi za ndege ili wakimbie wakisababisha fujo nchini

Hii hapa Tiketi namba TE 0717585676968 ya safari ya Lissu kumrudisha Ubelgiji alikotoka baada ya kufeli kwa jaribio lake la kutaka kutuletea vurugu nchini.

Lissu ataondoka Dar es Salaam International Airport Terminal Disemba 18, 2020 kuelekea Brussels Ubelgiji akipitia Addis Ababa Ethiopia kwa ndege ya shirika la ndege la Ethiopian Airlines

Ndege atakayopanda ni namba ET 804H itaruka hapa nchini saa kumi na dakika 45 jioni na atatua Addis Ababa saa Moja na dakika 25 usiku

Lissu ataondoka Addis Ababa kuelekea Ubelgiji saa tano na dakika 45 usiku  na atafika ubelgiji saa kumi na moja na dakika 15 alfajiri.

Kutokana na hilo kuimebuka mjadala katika mitandao ya kijamii watu wa kihoji uzalendo wa Lissu kutaka kuleta machafuko na kukimbilia nje ya nchi.

Tujitegemee ambaye ni mwanachama wa Matandao wa jamii forum alihoji, “Kwa hiyo Lissu bado hajapona!!! Sasa Watanzania hawawezi kumchagua Mtanzania ambaye ni mgonjwa kuwa Rais. Jukumu la urais linahitaji Mtanzania ambaye yupo sawia kiafya ili aweze kutimiza majumuku hayo kwa ufanisi. Watanzania sasa mnasababu nyingine ya msingi ya kutokumchagua Ndugu Lissu tarehe 28/10/2020.”

“MUONGO HUYO! Alipigwa risasi 16 za NDEGE na wenzake ndani ya chama chao kama sehemu ya kugombea madaraka ya UENYEKITI na pia kama njia ya kumfanya aende Ulaya kupanga huu mkakati wa kuja kuvuruga nchi, kwani ilikuwa vigumu sana kuyapanga haya wakati akiwa Bungeni , akiendelea na Ubunge wake; kwani asingeweza kutoka kwa muda mrefu waliokuwa wakihitaji hao mabeberu kwa ajili ya “kumtengeneza na kumtayarisha” kwa kuvuruga uchaguzi wetu. Pia walihitaji muda wa kutosha kwa ajili ya kumwekea vyuma na vifaa vya mawasiliano mwilini mwake, kumhakikishia pesa za uchaguzi, pesa za kuishi yeye na familia yake na pia makazi mapya baada ya kukamilisha MISHENI yake hapa nchini. Misheni ambayo IMEMSHINDA.

Na siku za nyuma tuliwambia kuwa mwenzenu anayo makazi Ubelgiji, mkatutukana humu JF lakini leo Lissu kategua hicho kitendawili. HALAFU nauliza kweli Serikali inaweza kumpiga mtu risasi namna hiyo ILI IWEJE? Sielewi naomba ufafanuzi wa hili jamani.”alisema Mukaruka Mzee katika mtandao huo.

Zandrano aliandika katika ukarasa huo maarufu nchini kwa masula ya siasa, “Lissu acha kuudanganya wananchi, kama kweli ulipigwa risasi kwa Amri yake kwanza usingerudi tena Tanzania, lakini kama haitoshi tangu ulivyorudi ulivyoshuka uwanja wa ndege ulisindikizwa chini ya ulinzi wa Askari wa Tanzania hadi nyumbani kwako, kama haitoshi Mikutano yako yote ya kampeni hadi unapolala unalindwa na Askari wa Tanzania, hili linawezekanaje?! kweli wewe ungeamini kulindwa na wabaya wako waliokukosa?!?! Lissu unadanganya watanzania na dunia kwa ujumla, ulipo lazwa Nairobi viongozi hao hao unaowatuhumu walikuja hadi hospotali kukujulia hali na wewe ulikubali waruhusiwe kuja kukuona!!! Ilikuwaje wabaya wako waliotaka kukuua uwaruhusu kuja kukona hospitali?!! Inawezekanaje!! Huo ni uongo mtupu!!”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here