Thomas Ulimwengu aipeleka TP Mazembe hatua ya makundi

0

Hizi ndio zilizofuzu hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika

KINSHASA, DR.CONGO

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu juzi amefunga bao la kwanza dakika ya 14, TP Mazembe ikiibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Bouenguidi FC ya Liberia katika mchezo wa marudiano Hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa TP Mazembe Jijini Lubumbashi.

Ushindi huo, unaifanya TP Mazembe kuungana na miamba mingine ya soka barani afrika katika 16 Bora ambazo zitashiriki katika hatua ya makundi.

Bao la pili la Mazembe katika mchezo huo lilifungwa Mzambia Tandi Mwape dakika ya 45, wakati bao pekee la Bouenguidi FC lilifungwa na Djoe Dayan Boussougou dakika ya 79 na sasa wanakwenda hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Mechi ya kwanza pia Ulimwengu alifunga mabao mawili Jijini Libreville, Mazembe wakishinda 2-1 pia.

Aidha, orodha kamili ya miamba hiyo 16 iliyotinga hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika 20/21 ni: Zamalek (Misri), Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini), Kaizer Chiefs (Afrika Kusini) na Al Ahly (Misri).

Wengine ni Teungueth FC (Senegal), CR Belouizdad (Algeria), TP Mazembe (DR Congo), MC Alger (Algeria), Espérance Tunis (Tunisia), Simba SC (Tanzania ) na Al Merrikh SC (Sudani)

Pia wamo, As Vita Club (DR Congo), Al Hilal Cl (Sudani), Wydad AC (Morocco), Horoya AC (Guinea) na Petro Atletico (Angola).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here