Tembo 170 kupigwa mnada Namibia

0

Windhoek, Namibia

KIANGAZI na mgogoro kati ya wanyama na binadamu imefanya Namibia kuuza tembo 170 kwa mnada.

“Kwasababu ya ukame na kuongezeka kwa idadi ya tembo, na mgogoro kati ya tembo na binadamu, kumetambulika haja ya kupunguza idadi ya wanyama hao,” kwa mujibu wa tangazo lililowekwa katika gazeti la New Era linalomilikiwa na serikali.

Tangazo hilo lililowekwa na wizara ya mazingira ni zabuni ya kutafuta kampuni inayofikia mahitaji yanayotakikana ikiwemo viwango vya kimataifa na kibali cha usafirishaji wanyama.

Wanaotaka kutuma maombi wana hadi januari 29 kufanya hivyo.

Mwaja jana, nchi hiyo iliidhinisha uuzaji wa karibu wanyama 1,000 ambao walikuwa katika hatari ya kufa kwasababu ya ukosefu wa chakula.

Wanyama waliokuwa wanauzwa ni pamoja na tembo, nyati, twiga na pala lengo likiwa ni kupatikana kwa dola milioni 1.1 kwa ajili ya uhifadhi wa mazingira.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here