Teknolojia mpya kutumika kupanda Mlima Kilimanjaro

0

Kamishina msaidizi wa Uhifadhi wa TANAPA, ACC Paul Banga amesema General Management Plan(GMP) ambayo inahusisha Wadau wote wa Utalii, walipitisha mpango wa kuanzisha cable car katika Mlima Kilimanjaro ikiwa ni mkakati wa kuongeza idadi ya Watalii nchini. Aliyasema hayo wakati wa kikao cha Tanapa na Wahariri na Waandishi wa habari waandamizi Jiji Dodoma.

Banga amesema Cable car hiyo itaanzia karibu na Geti la Machame la kupandia Mlima Kilimanjaro na kuishia Uwanda wa Shira. Cable car itakuwa na Urefu wa mita 3,700 kati ya mita 5,895 za Mlima Kilimanjaro. Car cable haitafika kwenye Kilele cha Mlima Kilimanjaro

Amesema kwa sasa Serikali bado inafanya tathimini kuona kama mradi wauruhusu au wasiuruhusu.

Kutoka na hofu ya watu wengi kupoteza ajira hasa wasaidizi wa wapanda Mlima, alifafanua kwamba kazi za kupanda mlima kwa mguu zitaendelea kama kawaida kilichoongezeka ni kumuwezesha Mtalii kiwa na Chaguo la Atumie Miguu au car cable.

Banga alisema anatumbua uwepo wa Walemavu na Wazee ambao wanatamani kupanda Mlima Kilimanjaro hivyo cable car itasaidia kutimiza ndoto zao.

Cable car ni gari linalotumia waya kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine bila kugusa ardhi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here