TCRA yaifungia Wasafi TV miezi sita

0

Na Bethsheba Wambura

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeifungia kwa miezi sita Wasafi TV kwa kosa la kukiuka kanuni za utangazaji katika matangazo yake ya moja kwa moja ya Tamasha la Tumewasha.

Uamuzi wa kufunga Kituo hicho umefikiwa leo Jumanne Januari 6, 2020 baada mamlaka hiyo kukutana na uongozi wa Wasafi Tv na kusikiliza utetezi wao.

Kaimu Mkurugenzi wa TCRA Johanes Kalungule amesema ukiukwaji huo ulifanyika Januari 1, 2021 ambapo televisheni hiyo ilirusha maudhui yaliyomuonyesha msanii Gigy Money akicheza katika mitindo iliyoonyesha utupu wake.

“Kosa hilo ni kinyume na kanuni za utangazaji hivyo kuanzia muda uliotolewa uamuzi huo Wasafi Tv imetakiwa kusitisha matangazo yake na kuomba radhi mfululizo.

“Pia TCRA imesitisha utoaji wa huduma za utangazaji za Wasafi Tv kwa muda wa miezi sita kuanzia Januari 6, 2021 hadi Julai 6,” amesema.

Aidha Kalungule amesema iwapo Wasafi Tv itakaidi uamuzi huo hatua zaidi za kisheria na za kiuthibiti zitachukuliwa dhidi yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here