Tarimba: Kampuni za ‘betting’ zidhamini vilabu Tanzania

0

NA MWANDISHI WETU

MKURUGENZI wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tarimba Abbas amesema kuwa wakati umefika kwa serikali kuzitaka Kampuni za michezo ya kubashiri (Betting), nchini angalau kudhamini klabu moja ya mpira wa miguu ili nazo zinufaike na makampuni hayo ambayo yanajipatia pesa kupitia soka.

Tarimba Abbas aliyasema hayo, jijini Dar es Salaam juzi, wakati alipokuwa akikabidhi mfano wa hundi ya Sh. Mil. 23 kwa Mwenyekiti wa Namungo FC, Hassani Zidadu kama mchango wa SportPesa kukamilisha safari yao kuelekea mechi ya Sudan dhidi ya Al Hilal Obayed.

”Kampuni za Betting zinarudisha nini kwenye mchezo wa Mpira wa Miguu, miaka miwili iliyopita nimekuwa nikizungumza na viongozi wa kiserikali kuhusiana na swala hili …. ndiyo tunalipa kodi sawa lakini tunaufanyia nini Mpira wa Miguu ?,”alisema Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tarimba Abbas.

”Nipeleke hoja binafsi Bungeni ama kushawishi Waziri wa Michezo na Waziri wa Fedha kwamba Masharti ya Leseni ya kuendesha michezo ya kubashiri (Betting) iwe lazima kwa Kampuni kudhamini Mpira wa miguu, iwe ni kwa klabu za Ligi Kuu, Ligi daraja la kwanza ama la Pili.”

Tarimba ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kindoni ameongeza kuwa ”Kama klabu zetu za Ligi Kuu na ligi nyingine zitaweza kujimudu vizuri sana kwenye uendeshaji na kwenda katika mashindano na kuwa na wachezaji waliyo bora ni dhahiri kabisa hata timu yetu ya taifa tutakuwa na wachezaji wazuri.”

”Kuna kampuni karibu 23 za Bettingi hapa Tanzania na timu za Ligi Kuu zipo 18 inamaana hakuna timu ambayo ingekosa Udhamini na zikabakia Kampuni nyingine zikadhamini Ligi daraja la kwanza na la Pili. Timu zetu zifaidike kutokana na kazi wanazofanya, hizi Kampuni za Kubashiri wanatumia (Product za Football) iwe ligi ya nje ama ya hapa nyumbani wanatumia wakati timu hizi zikitoka jasho, hizi kampuni zinarudisha nini kwenye mpira wa miguu

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here