Tanzania Prisons waapa kuvunja rekodi ya Yanga

0

NA SHEHE SEMTAWA

MAAFANDE wa Jeshi la Magereza ‘Tanzania Prisons’ wameapa kuvunja rekodi ya Yanga ambao hawajafungwa tangu Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2020/21 ulipoanza mwezi Septemba.

Ikumbukwe kesho (Desemba 31), Tanzania Prisons yenye alama 21 ikiwa nafasi ya 11, itakua wenyeji wa Yanga inayoongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa alama 43, kwenye Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.

Katibu mkuu wa Tanzania Prisons Ajabu Kifukwe, alisema mbali na kupanga kuvunja rekodi ya Yanga, pia watautumia mchezo huo kulipa kisasi cha kuharibiwa rekodi yao ya kutopoteza mchezo hata moja kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita, na sasa amedai kuwa ni zamu yao.

Alisema, anaamini kuwa mchezo wa kesho hautokuwa rahisi, lakini na wao pia ni timu nzuri na wamejipanga kukabiliana na Yanga ambayo imemaliza mzunguko wa kwanza bila kupoteza mchezo hata moja, ikicheza michezo 17, ikishinda 13 na kutoka sare nne na ndiyo inayoongoza kwenye msimamo wa ligi mpaka sasa.

“Yanga haijapoteza mechi, sisi tumejipanga kuwa timu ya kwanza kuifunga na kuharibu rekodi hiyo kama walivyotufanyia wao msimu uliopita,” alisema Ajabu Kifukwe.

Msimu uliopita, Prisons ilikuwa timu pekee kwenye Ligi Kuu ambayo ilicheza michezo 12 bila kupoteza, kabla ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga.

Baada ya kushinda michezo minne na kutoka sare minane, Tanzania Prisons ilichapwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa Desemba 27, mwaka jana kwa bao la Mnyarwanda, Patrick Sibomana.

Kocha Mkuu wa Yanga, Cedrick Kaze, alisema anatambua kuwa mchezo huo utakuwa mgumu lakini wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya timu hiyo.

Mchezo huo ni wa kwanza kwa mzunguko wa pili msimu wa 2020/21 baada ya mzunguko wa kwanza kumeguka.

Yanga ilifunga pazia la mzunguko wa kwanza ikiwa imekusanya jumla ya pointi 43 ipo nafasi ya kwanza na haijapoteza mchezo hata mmoja.

Itakutana na Tanzania Prisons, kesho ikiwa ni mchezo wao wa mwisho kwa mwaka 2020 kabla ya kuanza mwaka mpya 2021 kwa Neema ya Mungu.

Kaze, alisema:”Wachezaji wapo vizuri na mazoezi ambayo wameyafanya ni mazuri yananipa picha kwamba tunakwenda kupata matokeo ugenini,”.

Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa, ngoma ilikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1, ilikuwa ni mechi ya kwanza na ya mwisho kwa Farouk Shikalo kukaa langoni kwa mzunguko wa kwanza

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here