Taifa Stars waanza mazoezi kujiandaa na mechi za kirafiki na chan 2021

0

NA SHEHE SEMTAWA

TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeanza mazoezi ya kujiandaa na mechi mbili za kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Watu wa Co (DRC), namichuano inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee (CHAN) nchini Cameroon.

Tanzania imepangwa Kundi D pamoja na Zambia, Guinea na Namibia.

Yapo makundu mengine ambayo ni kundi linaundwa na Cameroon, Mali, Burkina Faso na Zimbabwe, Kundi B; Libya, DRC, Kongo na Niger na Kundi C lina mabingwa watetezi Morocco, Rwanda, Uganda na Togo.

Hawa hapa ni baadhi ya wachezaji Stars ambao wameanza mazoezi mwishoni mwa wiki.

1. BEKI mpya wa timu ya soka taifa ya Tanzania, Taifa Stars akiwa mazoezini juzi, Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kujiandaa na michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Januari 10 na 13.

  1. Kiungo Feisal Salum akijiandaa na mechi hizo ni mechi maalum za Taifa Stars kujiandaa na Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN),  zitakazofanyika nchini Cameroon kuanzia Januari 16 hadi Februari 7, mwaka huu.

  1. Kiungo Farid Mussa akijiandaa na CHAN, michuano inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee, Tanzania imepangwa Kundi D pamoja na
    Zambia, Guinea na Namibia
  2. Beki Bakari Mwamnyeto akijifua na kujiandaa na CHAN, michuano inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here