Taifa Stars kuiduaza Tunisia nyumbani kwao leo

0

 >>Inaniuma kuikosa Tunisia lakini sina namna-Samatta

NA SHEHE SEMTAWA

UONGOZI wa timu ya Tanzania ‘Taifa Stars, umesema kikosi kipo tayari dhidi ya wenyeji wao Tunisia katika mchezo wa Kundi ‘J’, maalumu wa kufuzu fainali za kombe la Mataifa ya Africa (AFCON)  AFCON ya 2021 Cameroon.

Mechi hiyo itachezwa leo Ijumaa Uwanja wa Hamadi Agrebi Olimpiki mjini Rades, kabla ya timu hizo kurudiana Dar es Salaam siku nne baadaye na mechi zote zitaonyeshwa LIVE na chaneli ya ZBC 2 inayopatikana katika kisumbusi cha Azam TV.

Akizungumzia mchezo huo, Meneja wa Stars, Nadir Haroub ‘Canavaro’ alisema wachezaji wote wana morari ya hali ya juu ya kufanya vizuri katika mchezo huo wa leo.

“Kila mmoja anahamu ya kucheza katika wetu mchezo wa leo na wachezaji wana morali kubwa sana, kinachotakiwa ni kusubiri tu maamuzi ya mwalimu kupanga nani ataanza lakini kila mchezaji anahamu ya kucheza katika mchezo huo.

“Vijana wote wako fit, nawaomba Watanzania watuombee dua kwa sababu dua zao insha’Allah zinaweza zikatufikia na zikatusaidia vile vile.

“Ninachowaomba waendelee kutuombea dua ili tuweze kufanya vizuri kwa sababu hii ndio timu yaona hii, na wao ni mashabiki wetu hakuna wengine zaidi ya wao,”alisema Canavaro.

Canavaro, alisema, wachezaji na viongozi walio safari na timu wanajua kuwa wamebeba mzigo mkubwa na matarajio ya ushundi kwa Watanzania walio baki nyumbani.

“Ili tufanye vizuri katika mchezo wa leo lazima tucheza kwa bidii na bidii ni dua zao ambazo watatupa sisi nadhani vijana watafanya, tutapambana na tunaweza tukapata ushindi Insha’Allah,”alisema Canavaro.

Akizungumzia kukosekana kwa Nahodha Mbwana Samatta katika mchezo huo, Canavaro alisema Samatta ana umuhimu kwenye timu hiyo kama mchezaji wa taifa.

“Lakini mchezaji akipata majeruhi ina maana lazima utafute mbadala amabaye anaweza akaitumia nafasi yake na kuweza kufanya vizuri.

“KUsema ukweli tuna pengo, Samatta ni mchezaji mmoja muhimu sana lakini sio kama Samatta hayupo timu isiweze kucheza ah! Hapana,”alisema Canavaro.

Canavari, alisisitiza kuwa walio kuwepo watapata nafasi na watajituma na wanaweza wakaleta matokeo mazuri katika kikosi hicho.

Kocha Mkuu wa Stars Ndayiragije, alisema kuwa kutokana na maandalizi ambayo wameyafanya wana imani ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa huo wa kufuzu Afcon leo.

Ndayiragije, alisema katika mchezo huo atawakosa washambuliaji wawili ambao ni pamoja na Adam Adam ambaye alikosa paspoti ya kusafiria pamoja na Nahodha ambaye anasumbuliwa na maumivu ya msuli.

Kocha huyo amesema:”Kila kitu kipo sawa kwa maandalizi ambayo tumeyafanya nina amini kwamba tutapata matokeo chanya licha ya kwamba tutakuwa ugenini.

“Kikubwa tunatambua kwamba hatutakuwa na Samatta ila wapo wachezaji wengine ambao watacheza kwa niaba yake na nina amini kwamba watapambana ili kufanya vizuri kwani matokeo yakiwa mazuri ni furaha kwa kila mmoja,”Ndayiragije.

Stars ipo kundi J ina pointi tatu ikiwa inakutana na Tunisia ambao ni vinara wakiwa na pointi sita hivyo ikishinda itaongeza nafasi ya kunusa hatua ya kufuzu Afcon 2021 nchini Cameroon.

Naye Samatta, atakosekana katika mchezo huo, wa kwanza wa kufuzu fainali za kombe hilo la AFCON, kufuatia majeraha aliyoyapata wakati akitumikia klabu yake ya Fenerbahce ya Uturuki.

Samatta alipata majeraha hayo wiki iliyopita katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Uturuki dhidi ya Klabu ya Konyaspor ambao ulimalizika kwa Fenerbahce kufungwa mabao 2-0.

Akizungumzia majeraha hayo, Samatta alisema kuwa amefanyiwa vipimo anatakiwa kuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya siku 10 kwa ajili ya kuipumzisha misuli ili irejee katika hali yake ya kawaida.

“Mechi ya mwisho ya ligi nilipata maumivu ya misuli na nilifanyiwa vipimo na majibu yametoka mabaya; natakiwa kuwa nje kwa zaidi ya siku kumi.

“Na ripoti ya daktari inaeleza napaswa kupumzika ili misuli irejee katika hali ya kawaida, imeniumiza sana lakini sina namna, nilitamani kuwepo kama kiongozi wa timu.

“Lakini sina namna ila nimekuja kuongea na vijana na Mwalimu nijue hali yao ikoje,” alisema Samatta kabla ya Stars kuondoka Uturuki juzi kuelekea Tunisia.

Mchezo wa kwanza wa timu ya Taifa ya Tanzania wa kufuzu Afcon dhidi ya Tunisia utapigwa leo Novemba 13, 2020 mjini Tunis, na mchezo wa marudio utachezwa Novemba 17, 2020 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mechi zote mbili, Samatta atakosekana kwa kuwa bado atakuwa kwenye chini ya uangalizi wa madaktari.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here