Taasisi za umma zinazodaiwa na TTCL kikaangoni

0
Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba akifafanua jambo kwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (wa kwanza kulia) kuhusu mitambo ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano wakati wa ziara yake kwenye Shirika hilo, Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Kundo Mathew

NA AZIZA MASOUD,DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk.Faustine Ndungulile ametoa mwezi mmoja kuhakikisha wizara na taasisi za serikali zinazodaiwa na Shirika la Mawasiliano la Simu TTCL kulipa madeni yao ambayo ni zaidi ya Sh Bilioni 30 kabla ya maene hayo hayajasitishiwa huduma.

Dk.Ndungulile ametoa kauli hiyo jana alipofanya ziara katika shirika hilo ambalo lipo chini ya wizara hiyo mpya kwa lengo la kufahamiana na kusikiliza changamoto zilizopo

Alisema taasisi na wizara hizo ambazo zipo zaidi ya 20 zinapaswa kuandikiwa barua na Mkurugenzi ambazo zitawakata kila mmoja kulipa deni analodaiwa ifikapo Januari 31 mwakani.

“Taasisi zinazodaiwa zote zinapaswa kulipa fedha hizo zinazotokana na huduma wanayopatiwa ifikapo Januari 31 baada ya hapo nitachukua hatua yakusitisha huduma ikiwemo kukata mawasiliano katika maeneo husika,”alisema Dk.Ndungulile.

Alisema ni muhimu wizara na taasisi hizo kuzingatia suala hilo kwakuwa shirika linatumia gharama kubwa kujiendesha ikiwemo kuendesha mkongo wa Taifa.

Mbali na hilo Dk.Ndungulile pia alisema serikali imebaini hujuma zinazofanyika katika mkongo wa Taifa za baadhi ya watu kuiba nyama na kwenda kuyeyusha kutengeneza madini ya kopa jambo ambalo linaosababishia shirika hasara.

“Kuanzia sasa naenda kuongea na vyombo vya ulinzi na usalama kuwaelekeza ikitokea mtu yoyote kakamatwa na hizi nyaya ana kopa ambayo haijulikani chanzo chake ataingia kwenye orodha ya wahujumu uchkumi,”alisema Dk.Ndungulile.

Pia Dk.Ndungulile alitoa tahadhali kwa watia huduma za mtandao ambao wanahujumu mitambo ya TTCL ili isifanye kazi vizuri na kuahidi kuwashughulikia.

“Kampuni zinazoihujumu TTCL nazijua na sitozitaja,nawapa taarifa tunajua wanachofanya hizi salam ziwafikie tutawachukulia hatua kali,”alisema Dk. Ndungulile.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa TTTCL Waziri Kindamba aliahidi kufanyia kazi maagizo yaliyotolewa na Waziri na kuwataka wafanyakazi wa shirika hilo kufanya kazi kwa bidii na kuacha mazoea.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew akisisitiza
jambo kwa wafanyakazi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (hawapo pichani) wakati wa
ziara ya Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Faustine Ndugulile (anayesikiliza) alipotembelea Shirika
hilo, Dar es Salaam.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here