Taasis ya Kilakona yaja na Teknolojia mpya ya ufundishaji mashuleni

0

Na Mwandishi Wetu

KATIKA kuhimiza matumizi ya teknojilia ya ufundishaji kwa shule za awali ,msingi na Sekondari nchini, taasisi ya ‘Kilakona Initiatives’ imezindua mfumo ‘App’ inayowawezesha wanafunzi wa shule hizo kufundishwa masomo mbalimbali kwa njia ya kiteknolojia.

Mfumo huo unaotambulika kama ‘Kilakona Schools’ unaopatikana kwenye ‘Play Store’ mbali na kutumika katika ufundishaji, pia unamwezesha mzazi kufuatilia mwenendo wa maendeleo ya mtoto wake kuanzia anapotoka nyumbani, awapo darasani hadi anaporejea nyumbani.

Akizungumza wakati wa kuwasilisha maelezo wa mfumo huo kwa wakuu wa shule za msingi na awali kutoka shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Taasis hiyo, Salim Mngodo, alisema kuanzishwa kwa mfumo huo kutazidi kuchochea maendeleo ya kielimu nchini hususani kipindi hiki ambacho teknolojia inazidi kukua kwa kasi.

Alisema kutokana na maendeleo ya kiteknojia nchini na uliwenguni kwa ujumla, taasisi yake iliona vyema kuja na mfumo huo kwa ajili ya kurahisisha kazi ya ufundishaji kutoka kwa mwalimu kwenda kwa mwanafunzi wakati wowote awapo shuleni au nyumbani jambo linaloweza kuchangia uelewa kwa haraka kwa mwanafunzi huyo.

“Mfumo huu una msaada mkubwa katika kuwaunganisha mwalimu na mwanafunzi wake, hata kipindi cha janga la Corona, uliweza kuwasaidia wanafunzi wengi kuendelea kusoma wakiwa majumbani kupitia simu za wazazi wao hususani kwa shule zilizounganishwa na mfumo huo” alisema Mngodo

Alisema kwa sasa mfumo huo unaotumika katika baadhi ya shule za awali na sekondari za binafsi, umezidi kutoa matokeo chanya kwa kuonyesha maendeleo mazuri kutokana na wanafunzi wengi konekana kuuelewa zaidia, na hivyo kuendelea kuwafikia wanafunzi hata baada ya muda wa masomo wakiwa majumbani.

Kwa upande mwingine Mkurugenzi huyo alisema mfumo huo wa ‘Kilakona Schools’ pia unamsaidia mzazi kufuatilia maendeleo ya mtoto wake, kuanzia awapo njiani, shuleni na hata kufahamu juu ya alichofundishwa, mazoezi aliyopewa, majaribio na hata matokeo ya mitihani alipokuwa shule na kwa namna gani ameweza kuelewa kile alichofundishwa.

Alisema kwa sasa wapo katika mpango wa kushirikiana na Serikali ili kuona namna ambavyo wataweza kuingiza mfumo huo katika shule za Serikali ambapo kwa kuanza Mkurugenzi huyo alisema wapo katika mpango wa kuzitumia shule mbili za kata zilizopo jijini Dar es Salaam ambazo zina matokeo mabaya kitaaluma ili kuona namna teknolojia hiyo itakavyobadirisha matokeo yao kitaaluma

Mkurugenzi wa Kilakona Schools, Salim Mngodo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here