Subhash Patel afariki dunia

0

Mfanyabiashara na mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya Motisun Group, Subhash Patel amefariki dunia leo Jumanne Desemba 15, 2020.

Kampuni ya Motisun inamiliki hoteli maarufu nchini Tanzania za White Sands na Sea Cliff na ndio wazalishaji wa juisi na maji chapa ya Sayona, saruji chapa Mamba. Bidhaa nyingine maarufu ni rangi, mabati na matangi ya kuhifadhia maji ya chapa Kiboko.

Kampuni hiyo pia ina mtandao wa biashara nchini Msumbiji, Zambia na Uganda.

Watu mbalimbali wametuma salamu za rambirambi akiwamo mfanyabiashara Mohamed Dewji ‘Mo’ kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii.

“Nimehuzunishwa na taarifa ya kifo cha  Subhash Patel aliyekua mtu wa kujitoa sana kwenye masuala ya jamii na kujali watu. Natoa pole kwa ndugu, jamaa na rafiki kwa namna ambavyo wameguswa na msiba huu. Mwenyezi Mungu amsamehe na kumjaalia pepo,” amesema Mo.

Naye Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter ameandika; “Tanzania imepoteza Mwana-Viwanda, Chalinze Imepoteza Mtoto na mwana Maendeleo. Najiandaa kuandika, nasita ila Nitaandika. Nilivyokufahamu, mapenzi kwa Chalinze kwenu, Tanzania na jinsi ulivyopokea Sera za Serikali ya Viwanda ya serikali ya Raisi Magufuli. Nakulilia Subhash.”

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here