Straika aliyewapa Italia Kombe la Dunia afariki 

0

ROME, ITALIA

MCHEZAJI wa zamani wa timu ya taifa ya Italia, Paolo Rossi amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 64.

Nyota huyo anakumbukwa zaidi baada ya kucheza kwa mafanikio makubwa hadi kupelekea kuipatia Italia Kombe la Dunia mwaka 1982.

Mbali na Italia lakini pia ‘legend’ huyo, Paolo Rossi aliyepata kuzitumikia klabu za  Juventus na AC Milan katika safu ya ushambuliaji amewahi kutwaa tuzo ya Golden Boot na Golden Ball mnamo mwaka 1982 huku akitwaa makombe 48.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari kutoka nchini Italia, Paolo Rossi amefariki Dunia baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here