Spika wa Bunge nchini DRC ang’olewa

0

Spika wa Bunge la DRC, Jeanine Mabunda ameondolewa katika nafasi yake baada ya Wabunge kupiga kura ya maoni dhidi yake iliyowasilishwa bungeni na Upinzani.

Miongoni mwa Wabunge 484 katika Bunge hilo walipiga kura na 281 kati ya hizo zilisema kwamba Kiongozi huyo wa muhimili huo mkubwa aondoke katika nafasi yake.

Zaidi ya Wabunge 200 kati ya Wabunge 500 waalifanya kikoa cha kupiga kura ya kumuondoa madarakani Jeanine kutoka chama cha Joseph Kabila, rais wa zamani wa nchi hiyo.

Mwandishi wa BBC, nchini DRC anasema ; Upande wa chama cha Kabila tayari kulikuwa na mzozo katika vyama vilivyokuwa vinamuunga mkono, hivyo hiyo inaweza kuwa sababu ya kuanguka kwao.

Na hatua inayofuata ni Waziri Mkuu kujiuzulu sasa kwasababu Rais atamchagua mtu atakayeunganisha vyama bungeni hivyo nia ya Rais kuvunja muungano huo.

Lakini kinachoshangaza inakuwaje spika huyo ashindwe kupata kura za kutosha kumtetea  wakati Wabunge wa chama chake ni wengi zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here