Ndugai achukua fomu kuwania tena Uspika

0

Na Dotto Kwilasa, Dodoma 

Zoezi la uchukuaji fomu za kuwania nafasi ya Spika na Naibu Spika limeanza leo Jijini hapa Katika ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambapo hadi sasa ambaye amekamilisha taratibu zote ni Mbunge mteule wa Kongwa, Job Ndugai.

Kwa mujibu wa Katibu msaidizi Mkuu wa Oganaizesheni CCM Taifa Solomon Itunda zoezi hilo limeanza rasmi leo huku akimtaja Spika anayemaliza mda wake Job Ndugai kuwa ndiye Mgombea pekee wa nafasi hiyo ambaye amekamilisha taratibu zote hadi sasa.

Aidha ametaja gharama za fomu hizo kuwa ni 500, 000 kwa kila fomu.

Akizungumza mara baada ya kukamilisha taratibu zote za kujaza na kurejesha fomu Ndugai amesema anawaomba watanzania wamuombee ili Chama chake kimteue kwa mara nyingine kugombea nafasi hiyo.

Licha hayo Ndugai amesema nafasi ya Spika inapendekezwa na vyama vya siasa hivyo; “Ikiwa chama changu kitanikubalia  kuwa spika wa bunge la 12 tutaongea na watanzania kwa Wakati huo juu ya Vipaumbele vyetu.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here