Sina mpango wa kuolewa-Isha Mashauzi

0

Na Mwandishi Wetu

Muimbaji wa taarab nchini Isha Mashauzi amefunguka kuwa kati ya vitu asivyofikiria kwa sasa ni suala zima la ndoa.

Isha ambaye ni mama wa mtoto mmoja alisema, baada ya kuingia kwenye ndoa mbili na kutoka kwa sasa anahitaji kutulia kwanza.

Alisema, endapo mipango ya Mungu itatimia atarejea kwenye ndoa ila kwa sasa hafikiria hilo.

‘Ukiniuliza mambo ya ndoa hapana kwa sasa..nipo busy na shughuli zangu..nahitaji kunipanga zaidi..Mungu akijalia hiyo ni mipango ya baadaye sana’ alisema Isha.

Haya hivyo Isha amekiri kuwa ana uzoefu mkubwa wa maisha ya ndoa na ndio sababu ameamua pia kujikita kwenye elimu ya mahusiano.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here