Simba yawatimua wapishi wawili

0

NA MWANDISHI WETU

KUNA tetesi kuwa Uongozi wa Klabu ya Simba umewaondoa wapishi wao wawili ambao walikuwa wakihusika katika kuwapikia chakula wachezaji wa timu hiyo.

Hivi karibuni Simba imewashtua mashabiki wao kufuatia matokeo ya kufungwa mechi mbili mfululizo kwenye ligi, ilianza kwa kufungwa bao 1-0 na Prisons kule Nelson Mandela, Sumbawanga kisha iliporejea Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, ikapigwa bao 1-0 na Ruvu Shooting.

Awali Simba ilitangaza kuachana na kocha wa makipa Muharami Mohammed na meneja Patrick  Rweyemamu. 

Aidha, taarifa zingine zinasema kuwa imewapiga chini Ally Shantra na Jacob ambao walikuwa kwenye kitengo cha habari.

 Tetesi kutoka ndani ya Simba, ni kwamba timu hiyo imefikia hatua ya kuwafuta kazi wapishi wawili kutokana na hofu ya hujuma kufanyika kwa wachezaji wao. 

Inadaiwa kuwa, Simba imeamua kuachana nao fasta na kusaka wengine ambao wanawaamini katika utendaji kazi wao kwa kuhakikisha wanawapikia chakula safi  wachezaji na benchi lao la ufundi.

“Simba imeachana na wapishi wao wawili kwa hofu ya hujuma kwenye ishu ya vyakula vya wachezaji, wamefanya hivi ili kuhakikisha kila kitu kinakwenda safi  kwa wachezaji na timu nzima kwa ujumla,” kilisema chanzo hicho.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here