Simba, Yanga wapigana vikumbo Stars

0

Na Mwandishi Wetu

NYOTA wa klabu za Simba na Yanga wanakutana nchini Uturuki kwa ajili ya kuweka kambi ya kumeshana na Tunisia Novemba 13.

Wachezaji hao ambao saba wanatoka Simba na saba wengine wanatoka klabu ya Yanga, wamekutana nchini Uturuki ikiwa ni siku tatu toka walipokutana kwenye mchezo wa watani wa jadi.

Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 wapo kwenye kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambayo inakazi ya kucheza na Tunisia Novemba 13.

Mchezo huo wa kuwania kufuzu michuano ya Afcon 2021 unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili kutokana na nafasi ndani ya kundi j.

Tunisia ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi sita na imeshinda mechi zote mbili huku Tanzania ikiwa nafasi ya tatu na pointi tatu.

Hawa hapa nyota wa Simba  waliopo ndani ya Stars ni Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein (Tshabalala), Jonas Mkude, Erasto Nyoni, John Bocco, Mzamiru Yassin na Said Ndemla.

Kwa upande wa Yanga, waliopo kwenye kikosi cha Stars:-Metacha Mnata, Deus Kaseke, Bakari Mwamnyeto, Abdallah Shaibu (Ninja), Ditram Nchimbi, Feisal Salum na Farid Mussa wote wa Yanga.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here