Simba yachezea kichapo Sumbawanga

0

         >> Yanga yaanza vizuri chini ya kocha mpya
 
NA MWANDISHI WETU

WAKATI Simba SC wakikubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons, uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga, Yanga wao wamefanikiwa kuichapa bao 1-0 Polisi Tanzania, Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana.

Ikumbukwe vigogo hivyo vya soka nchini vilikuwa vikicheza michezo yao ya mzunguuko wa sita huku Tanzania Prisons na Polisi Tanzania wakicheza mechi za mzunguuko was aba.

Kwa matokeo hayo Simba SC inaendelea kubaki na pointi zake 13, Yanga wakipanda hadai nafasi ya pili kwa alama 16 nyuma ya Azam FC wenye pointi 21 baada ya kucheza michezo saba na kushinda yote.

Katika mchezo wa Simba dhidi ya Prisons, timu zote zilianza mchezo huo kwa tahadhari kubwa huku kila upande ukisoma mbinu za mpinzani wake.
Mchezo huo, ulitawaliwa na matumizi ya nguvu nyingi kwa Tanzania Prisons waliwapa tabu Simba.

Hadi dakika 45 zinakamilika timu hizo zilikuwa hakuna mbabe alijipatia bao.
Bao pekee la Tanzania Prisons liliwekwa kimiani dakika ya 48, Samson Mbangula akiunganisha kwa kichwa pasi kutoka kwa mmoja wa wachezaji wenzake.

Simba ilipata bahati mbaya kunako dakika ya 14, baada ya beki wao Shomari Kapombe kuumia nakwenda nje huku nafasi yake kuingia Kenedy Juma.

Mchezo mwingine,  Yanga walifanikiwa kuondoka na pointi tatu kwenye dimba la Uhuru Jijini Dar es Salaam baada ya kufanikiwa kuinyuka Polisi Tanzania bao 1-0.
Timu zote zilikwenda mapumziko zikiwa hazijapata kitu ambapo katika kipindi cha pili Yanga ilionekana kulisakama lango la Polisi Tanzania baada ya kufanya mabadiliko ya baadhi ya wachezaji.

Mabadiliko hayo, wachezaji waliongia walionesha chachu ya ushindi, kwa Yanga kupata bao mnamo dakika ya 70 kupitia kwa kiungo wao raia wa Congo Mukoko Tonombe ambaye alipokea pasi murua kupitia kwa Farid Mussa na kuitendea haki pasi hiyo.

Hadi dakika 90 zinakamilika, Yanga walifanikiwa kuondoka na alama hizo tatu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here