Simba kupata Bil. 1.3

0

>>Ni baada ya kuingia hatua ya makundi

NA SHEHE SEMTAWA

ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba SC, Ismail Eden Rage amesema kitendo cha timu yao kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabigwa barani Afrika kutaisaidia timu hiyo kuvuna Sh Bil. 1.3

Ikumbukwe, kufanya vizuri kwa Simba kwenye mashindano hayo ya Klabu Bingwa Afrika kutasaidia kuongeza wingi timu za Tanzania ambapo jumla ya timu nne zitapata nafasi ya kushiriki katika mashindano ya Chama cha Soka Barani Afrika (CAF) kwa maana ya Klabu Bingwa na Shirikisho.

Rage aliyasema hayo, wakati alipofanya mahojiano na Kipindi cha michezo cha Sports Arena kinachorushwa na Wasaf FM, jana asubu.

Kwakuingia hatua hii ya makundi klabu ya Simba SC itajiingizia kitita cha fedha za Kitanzania Tsh Bilioni 1.3 kutoka CAF wakati ambapo bado fedha kutoka kwa Mdhamini wao Mkuu SportPesa kwa kufanikiwa kutika hatua hiyo.

“Kuingia hatua ya makundi tutavuna dola laki tano na hamsini ambazo ni sawa sawa na Bil.1.3 bado kuna hela za SportPes ambako nako najua kuna mamilioni kama sijakosea mia mbli na kitu kama sijakosea.

“Za CAF nazifahamu kwa sababu `zimewekwa kwenye kanuni na wameongeza zawadi kubwa sasa hivi, mwaka jana mshindi wa kwanza alikuwa anapata dola milioni 2.5.

“Lakini sasa itakuwa dola milioni nne ambazo ni takribani kama Bil. 10,”alifafanua Rage.

Rage, alisema Simba wanaweza kupata zaidi ya Shilingi Milioni 200 za Kitanzania kutoka kwa Mdhamini wao Mkuu SportPesa kama zikiwa mahususi kwa ajili ya kuipa hamasa timu hiyo.

Mwaka 2019 Kampuni hiyo ya SportPesa ambayo pia ni wadhamini wakuu wa Yanga SC waliwapatia Simba SC kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 50 kwa Simba kuingia hatua ya robo fainali, Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumzia mchezo huo, Rage alisema kuwa wachezaji walikuwa na morari kubwa kwenye mchezo wa juzi hasa kutokana na mashabiki na wanachama wao kuwapa hamasa na ahadi waliyoahidiwa na ‘Management’ ya timu hiyo.

Uongozi uliwaahidi kuwapatia bonasi ya Shilingi Milioni 250 kitendo kilichowafanya wachezaji hao kuelewa umuhimu wa mchezo huo dhidi ya FC Platinum ya kutoka nchini Zimbabwe.

Katika mchezo huo, Simba iliwasukumiza nje ya mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika FC Platinum kwa jumla ya magoli 4-1 na hivyo kujihakikishia kuingia katika hatua hiyo ya makundi.

Waliokuwa mwiba mkali kwenye ngome ya FC Platinum, alikuwa ni Erasto Nyoni akifunga goli dakika ya 39, Shomari Kapombe bao lake dakika ya 61, John Bocco na Chama wakifunga kwenye muda wa nyongeza kabla mpira kuisha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here