Sijawahi kuzuia nyimbo za WCB kupigwa Clouds FM- Tale

0

NA MWANDISHI WETU

Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Hamis Taletale  ambaye pia ni meneja wa Msanii Diamond Platnumz afunguka juu ya kutowahi kuzuia Media kupiga nyimbo za wasanii wa WCB.

Akizungumza jana kupitia XXL kinachorushwa na Kituo cha Clouds Fm, Tale alisema kuwa hawajawahi kuzia media yoyote kutokupiga ngoma za wasanii wao bali Media ya Clouds ndio walianza.

“Hatujawahi kuzuia media yoyote kucheza nyimbo za wasanii wetu, uhalisia ni kwamba nyie (Clouds) ndio mlianza, na ninajua mmewahi kutusapoti na mlishawahi kuamua kutokutoa sapoti,”alisema Tale.

Majibu hayo yalimuibua Mtangazaji wa XXL, Adam Mchomvu, ambapo alisema, “Hatujawahi kuacha kukusapoti,”

Babutale akaendelea, “Tukienda kwenye uhalisia mimi na wewe (Adam) tumeshawahi kukutana kabla hata Marehemu hajafa, ukaniambia Tale kwanini msikae na viongozi mkamaliza, nikakuuliza kwamba kwani tumekosa nini tuseme tumalize.

“Shida tulikuwa tunataka kujua kwa nini hawapigi tumekosa nini.” alimalizia Tale. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here