Shibuda awataka wagombea watakaoshindwa uchaguzi kukubali matokeo

0
NA DOTTO KWILASA,DODOMA
MWENYEKITI wa Baraza la Vyama Vya siasa nchini John shibuda amewataka wagombea  wa vyama vyote na wa ngazi zote kujiandaa kisaikolojia katika kukubali matokeo ya kushinda ama kushindwa .

Shibuda ambaye pia ni Mgombea wa Urais kupitia chama cha ADA-TADEA alisema mwanasiasa kamili ni yule anayekubali matokeo yoyote na kwamba kwa uelekeo wa hali ya kisiasa ilivyo nchini ,Mgombea wa Urais kupitia CCM, Rais Dk. John Magufuli ana nafasi kubwa ya ushindi ukilinganisha na wengine.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini hapa mwishoni mwa wiki,Shibuda alisema hiki ni kipindi cha kuelekea mwishoni mwa uchaguzi hivyo ni vyema wagombea wote wajiandae kisaikolojia katika kupokea matokeo na kuepuka kujihusisha kushawishi wafuasi wao kufanya vurugu.

“Wagombea wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wapo 15 na upande wa visiwani Zanzibar wapo 17 ,Kama ni timu za mpira kapteni wake anapaswa kuwa ni Dkt,John Magufuli.” Alisema Shibuda na kuongeza;

“Lazima wagombea wote wajiandae kisaikolojia kupokea tamu na chungu ya matokeo ya uchaguzi ,mtu asiye na subra ya kuongozwa hana sifa ya kuitwa kiongozi “.
Shibuda akiongea kwa niaba ya Baraza la vyama vya siasa nchini,aliwataka wagombea wa vyama vya siasa kubadilika kulingana na mazingira na kuwa waungwana kwa kukubali kupongezana hata baada ya kushindwa ili maisha mengine yaendelee.
Pamoja na hayo aliwataka wanasiasa wote nchini kuelewa kuwa kura za ushindi hazitokani na kigezo cha mahudhurio ya hadhara.
“Ndugu zangu niwaambie wazi hadhara sio kigezo cha ushindi,wapiga kura ni sawa na darubini hupenda kupambanua na kupima maelezo ya kila mgombea na mwisho anayefaa ndie anaepata chake,”alisistiza Shibuda.
Hata hivyo alisisitiza kuwa wapiga kura wanapaswa kufahamu kuwa sumu haiwekwi jikoni .
“Kwa hiyo sasa tuelewane kuwa wanasiasa wote na washiriki wote wa vyama vya siasa hasa ambao hawatapata ushindi kwa wagombea wao kumbekeni kwamba kuvunjika kwa jembe siyo mwisho wa uhunzi;
kwa hiyo sasa Kama Simba na yanga hupeana mikono baada ya kutofautiana katika kushindania ubingwa  wa Taifa vivyo hivyo hata siasa nawasubiri tupongezane kwa kutakiana Heri kwa matokeo machungu kwa utashi wa umma”alisema.
Pamoja na Mambo mengine shibuda aliwataka wapiga kura kutokiuka Sheria za uchaguzi kwa kukaa kulinda matokeo na badala yake wanapaswa kuiamini tume ya Taifa ya Ucgauzi (NEC) kwani ndiyo yenye mamlaka ya kutangaza mshindi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here