SHAKA:Tumpe JPM ushindi wa kimbunga

0

NA MWANDISHI WETU,MOROGORO

CHAMA  cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Morogoro kimewaomba watanzania kumpa kura za kizalendo ili aweze kupata ushindi wa kimbunga   mgombea  urais wa chama hicho Dk.John Magufuli  kwakuwa ni kiongozi  mchapa kazi,mwenye huruma na upendo kwa watu wake.

Kimesema kuwa  kiongozi huyo kichwa chake kikichemka kuweka mipango na mikakati ya kuliletea Taifa maendeleo endelevu   na kwamba kupata kiongozi wa namna hiyo  ni jambo kubwa la kumshukuru  Mungu kwakuwa ni kama ameongeza  Tunu  nyingine ya Taifa.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Shaka Hamdu Shaka kwa nyakati tofauti  akiomba kura za Rais Magufuli, mgombea ubunge jimbo la Mikumi Denis Londo pamoja na madiwani wa kata za Mikumi, Tindiga, Ulaya, Ruaha na Kilangali wilayani Kilosa.

Alisema  Rais Dk. Magufuli katika kulitumikia Taifa  ametimiza wajibu wa kutumikia nchi na wananchi ambapo  amesimamia na kuleta maendeleo kisekta na kujenga uchumi imara hivyo bila na kuwataka watanzania bila kujali itikadi zao za kisiasa wampe kura Oktoba 28, mwaka.

“Lazima tumpe ushindi mnono Magufuli  na wa kimbunga 28 oktoba 2020 baada hapo tutaeshimiana, watani zetu watajua kuwa  CCM ni  kinara,  kielelezo na   alama ya Maendeleo Tanzania  na Afrika kwa ujumla inapobeba dhamana kwa wananchi wake” alisistiza Shaka

Alifafanua  kuwa utendaji wa kisera wenye tija na ufanisi alionesha Rais Magufuli ni kutokana na utekelezaji ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2015/2020  ambapo imeonyesha wazi wazi kwamba watanzania tutampigia Magufuli  kura nyingi za uzalendo kutokana na uaminifu wake hasa katika kulinda rasimali za taifa ambazo zimekuwa kichocheo kikubwa cha kuinua uchumi nchini.

“Hawana ajenda ya kujenga utaifa wamekuwa wakisema nikipata nitafanya wakati wananchi mnaona  maendeleo kwa macho yenu yaliyofanyika na yanayofanyika,wasifikirie watanzania ni wajinga hadi waridhie kuiacha nchi yao mikononi mwa fisi waliopandikizwa fikra za ukoloni mamboleo ili wakishika madaraka wakwapue rasilimali za Taifa na kuiacha nchi ikibaki ombaomba” alisema Shaka.

Alisema kwa mkoa wa Mororgoro kazi kubwa inayofanyika ni kupita kuomba kura za Magufuli na wanamini atashinda kwa kiwango kikubwa ili iwe fundisho kwa walioamua kuchapia kutafuta nafasi hiyo bila kujipanga nankujiandaa namna ya kutangaza sera zao ili watanzania waweze kuwamini na kuwapa ridhaa.

“Kazi si kutaka urais bali kazi kubwa ni kuutumikia Urais kama anavyofanya Rais Magufuli wengine wasubirie watanzania hawajafikiria kucheza bahati nasibu katika nafasi ya Urais wa nchi ni imani yetu tutashinda kwa kura zisizo mfano kwa vile imani ya wanatanzania kwa CCM na mgombea wake ni kubwa.” Alisema Shaka.

Pia  aliwataka wananchi wa jimbo hilo la Mikumi pamoja na kumpa kura Rais Magufuli wamchague Denisi Londo awe mbunge wa jimbo hilo  kwakuwa ni mtu hodari,  mzalendo na kwamba  atakuwa ni  mtumishi wao katika kupigania na kusimamia maendeleo.

“Londo sio gunzi bali  atakuwa ni kiungo kati Rais Magufuli , Serikali Kuu, Halmashauri, vijiji na vitongoji katika kusimamia maendeleo endelevu ambayo yawezekana kwa miaka mitano mliyakosa kutokana na kukosa mtu madhubuti wa kuwasemea, kuwasimamia na kuwapigania wana Mikumi katika mambo ya msingi yanayogusa maisha yenu ya kila siku” alisema Shaka

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here