Seven Mosha bosi Sony Music Africa Mashariki

0

WASHINGTON, MAREKANI

SONY Music Ent. Afrika imemteua Christine Mosha maarufu Seven, kuongoza upande wa Masoko na Maendeleo ya Wasanii kwa Ukanda wa Afrika Mashariki.

Mosha ambaye ni Mtanzania atakuwa na jukumu la kuijenga Kampuni hiyo ikiwemo kukuza Wasanii wa Afrika Mashariki na kuwafanya wafanye vizuri ndani na Nje katika level za Kimataifa.

Kwa mujibu wa  Sony Music Ent. Afrika, Seven atakuwa anaripoti moja kwa moja kwa Sean Watson, Managing Director wa Sony Music Afrika.

“Seven ametumia karibu maisha yake yote kutoa mchango kwenye Muziki wa Afrika , ana passion na anafaa kuutangaza Muziki wa Afrika Mashariki kwenye Ramani ya Dunia,”alisema Sean Watson.

Hivi karibuni Msanii Ommy Dimpoz alitangaza rasmi kuwa ameingia Mkataba na Sony Music Ent. Afrika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here