Serengeti yashinda tena tuzo hifadhi bora Barani Afrika

0

Na Bethsheba Wambura 

Hifadhi ya Taifa Serengeti imeshinda Tuzo ya kuwa Hifadhi Bora katika Bara la Afrika kwa mwaka 2020.

Tuzo hizo zimetangazwa jana Novemba 9,2020 na Taasisi ya World Travel Awards (WTA) ya nchini Marekani kwa njia ya mtandao ambapo Hifadhi ya Serengeti imeshinda Tuzo hiyo kwa mara ya pili baada ya kushinda mwaka 2019.

Taarifa ya ushindi huo imetolewa na Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Uhifadhi- Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Pascal Shelutete leo Jumanne Novemba 10, 2020.

Amesema Serengeti inajivunia umaarufu wa msafara wa Nyumbu wahamao zaidi ya milioni 1.5, aina mbalimbali za wanyamapori wanaopatikana kwa wingi, mandhari nzuri ya kuvutia pamoja ma shughuli za utalii zinazovutia watalii wengi.

“Hifadhi ya Serengeti imeibuka mshindi katika shindano hilo lililoshindanisha hifadhi tano: Central Kalahari(Botswana), Etosha (Namibia), Kidepo Valley(Uganda), Kruger (Afrika Kusini) na Maasai Mara Nationa Reserve (Kenya)” amesema Shelutete na kuongeza kuwa;

“TANAPA linaishukuru Serikali ya Tanzania, wadau wa utalii na wananchi wote waliopiga kura na kuifanya Serengeti kuwa mshindi.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here